WANANCHI WILAYANI PANGANI WATAKIWA KUJITOLEA KUCHANGIA DAMU
Wito umetolewa kwa wananchi wa wilaya ya pangani
kuwa na utaratibu wa kuchangia damu ili kupunguza vifo na adha mbali mbali
zinazotokana na upungufu wa damu
wilayani Pangani.
Wakizungumza na kituo hiki mara baada ya zoezi la
kuchangia damu lililofanyika katika eneo la standi ya mabasi mjini Pangani,
baadhi ya wananchi wamesema kuwa kuchangia damu kutawezesha wagonjwa wenye
uhitaji kuepukana na adha mbalimbali zinazojitokeza.
Mwananchi mmoja anayefahakima kama Bakari Rambazo
ambaye pia ni mchangiaji wa damu katika zoezi hilo amesema kuwa kuna faida
nyingi za kuchangia damu ikiwemo kuokoa maisha ya wagonjwa mbalimbali jambo
linalopelekea mchangiaji wa damu kupata thawabu kwa mwenyezi Mungu.
Naye mjumbe wa kamati ya damu salama kutoka katika
hospital ya wilaya ya Pangani ambaye ndiye aliyeendesha zoezi hilo Bwana Peter
Mshabaha amesema kuwa zoezi hilo limesuasua kwa kuwa wananchi wengi hawana
muamko wa kuchangia damu hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwani
zoezi hilo pia linasaidia mchangiaji kujua afya yake.
Zoezi la uchangiaji damu limekuwa likihamasishwa nchini
nzima kupitia serikali ili kuokoa maisha ya wagonjwa hususani wakina mama
wajawazito na watoto.
No comments