MDUDU ANAYEHUSISHWA NA UHURU WA TANZANIA AONEKANA PANGANI



Katika hali isiyotegemewa  mdudu wa jamii ya Barare anayehusishwa   na historia ya uhuru wa Tanganyika kulingana na alama ya namba tisa katika mabawa yake na baadhi ya rangi mbalimbali alizonazo mwilini ikiwemo rangi za njano na kijani.

Si kuamini kusikia,bali endapo utapata bahati ya kumshuhudia kwa macho yako,alipokuwa akizungumza na kituo hiki mkazi mmoja wa wilayani Pangani Bwana Mnyihaji Mzee Simba ambae ndie aliyemuokota mdudu huyu anaelezea historia yake na namna walivyokuwa wanapatikana mara baada tu ya uhuru wa Tanganyika.

Mbali na hayo nilitaka kufahamu zaidi endapo wadudu hawa waliokuwa wanonekana kipindi ambacho Tangayika ilipata uhuru mwaka 1961,je na huyu wa leo wanashabihiana na huyu kwa kiasi kikubwa Mzee Simba hapa anafafanu.

Tanganyika ilipata uhuru wake mwaka 1961 kwa mujibu wa maelezo ya Mzee Simba kipindi hicho kulikuwa na wadudu aina ya Barare ambao walikuwa na rangi zinazoshabihiana na bendera ya Taifa pamoja na alama ya namba Tisa mojawapo ya namba inayounda mwaka ambao Tanganyika ilipata uhuru.

No comments

Powered by Blogger.