WAKULIMA WILAYANI PANGANI WAJIPANGA KULIMA KILIMO CHA ALIZETI.




Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kuathiri uhakika wa kupata mavuno ya kutosha kwa baadhi ya mazao wilayani Pangani wakulima wilayani humo wamejipanga kuanzisha kilimo cha Alizeti ili kukabiliana na athari hizo na kujikwamua kiuchumi.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wakulima katika kijiji cha Sange wilayani humo ambapo Bwana Albano Peter Mwalido amesema kwa sasa wao kama wakulima wamehamasika kulima zao hilo kwakuwa limeonekana kuleta tija kwa wakulima wa mikoa mingine nchini Tanzania.

‘’Zao la alizeti mwanzo kabisa hatukuliwekea maanani na hata matumizi ya mafuta ya zao hili hatukuwa tukiyatumia sasa dunia ni pana watu wamelikubali nje na ndani ya wilaya yetu kilichobaki ni wakulima kuelimishwa namna ya ulimaji’’ amesema peter.




Kwa upande wake mkulima Mwengine aliyejitambulisha kwa jina la MATESO  JOHN amesema wakulima wengi katika wilaya ya Pangani wamechelewa kulima zao hilo kutokana  na kuhofia kutostawi katika maeneo yao huku akisema wakulima wengi wamejipanga kulima zao hilo kwa msimu ujao wa mwaka.

‘’Tangu asili tulipokuwa tunakuwa tulikuwa tunaona wazee wetu wakilima ufuta, mihogo na mpunga hili zao la alizeti tulikuwa tukilishuhudia kwa wenzetu tuu sasa tayari kwa pangani limeonekana lina tija, ninachowaomba wakulima waongeze nguvu yakulilima’’ amesema Mateso.

No comments

Powered by Blogger.