"HALMASHAURI YA PANGANI IMEJIPANGA KWA ZOEZI LA USAILI"- BI MWANAIDI RAMADHANI NONDO



Afisa Utumishi Wilayani Pangani Bi Mwanaidi Ramadhani Nondo amesema kuwa Halmashauri hiyo imejipanga vyema kwa ajili ya usaili wa nafasi za Watendaji wa vijiji pamoja na Makatibu Muhtasi utakaofanyika siku ya Jumamosi ya terehe 14 hadi 15 mwezi huu wa kumi.

Akizungumza na Pangani Fm mapema leo, Bi Mwanaidi amesema kuwa wanatengemea kupata maombi mengi kutoka kwa wananchi wenye vigezo kutokana na matangazo mengi ambayo yamesambaza maeneo mbali mbali.

“Ni matumaini yetu watakuja watu wengi, kwa kuwa pia tumeweka matangazo kwenye tovuti yetu ya Halmashauri, mbao za matangazo pamoja na kata zote za wilaya” alisema Bi Mwanaidi.

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa, kwa upade wa mwenyekiti wa bodi ya ajira wameshapeleka mapendekezo kwenye kamati ya fedha na kwa sasa wanasubiri baraza la Madiwani kupitisha huku akiwataka wananchi kutarajia usaili wa haki.

No comments

Powered by Blogger.