MDUDU ANAYEHUSISHWA NA UHURU WA TANZANIA AONEKANA PANGANI
Katika hali isiyotegemewa mdudu wa jamii ya Barare anayehusishwa na historia ya uhuru wa Tanganyika kulingana
na alama ya namba tisa katika mabawa yake na baadhi ya rangi mbalimbali
alizonazo mwilini ikiwemo rangi za njano na kijani.
Si kuamini kusikia,bali endapo utapata bahati ya
kumshuhudia kwa macho yako,alipokuwa akizungumza na kituo hiki mkazi mmoja wa
wilayani Pangani Bwana Mnyihaji Mzee Simba ambae ndie aliyemuokota mdudu huyu
anaelezea historia yake na namna walivyokuwa wanapatikana mara baada tu ya
uhuru wa Tanganyika.
Mbali na hayo nilitaka kufahamu zaidi endapo wadudu
hawa waliokuwa wanonekana kipindi ambacho Tangayika ilipata uhuru mwaka 1961,je
na huyu wa leo wanashabihiana na huyu kwa kiasi kikubwa Mzee Simba hapa
anafafanu.
Tanganyika ilipata uhuru wake mwaka 1961 kwa mujibu
wa maelezo ya Mzee Simba kipindi hicho kulikuwa na wadudu aina ya Barare ambao
walikuwa na rangi zinazoshabihiana na bendera ya Taifa pamoja na alama ya namba
Tisa mojawapo ya namba inayounda mwaka ambao Tanganyika ilipata uhuru.
No comments