BREAKING NEWS: MKURUGENZI WA PANGANI ASIMAMISHWA KAZI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa TAMISEMI kuwasimamisha kazi Wakurugenzi wa Halmashauri ya Kigoma Ujiji na Pangani kutokana na Wilaya zao kuwa na hati chafu katika ripoti ya CAG iliyowasilishwa leo Ikulu.

Rais Magufuli amewasimamisha kazi Wakurugenzi hao leo Ikulu jijini Dar es salaam, baada ya kupokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali(CAG), Profesa Mussa Assad.

“Wakurugenzi wa Halmashauri ya Kigoma Ujiji na Pangani wameandikiwa hati chafu, inabidi tuanze kuchukua hatua.Ninawasimamisha mara moja Wakurugenzi wa halmashauri hizi mbili kwa Waziri wa TAMISEMI yuko hapa kwahiyo Wakurugenzi wa wilaya hizo wasimamishwe kazi leo, inawezekana si vizuri sana ila inabidi tuchukue hatua,“ amesema Rais Magufuli.

Prof. Assad amesema serikali za mitaa 140 zilishindwa kukusanya mapato ya shilingi bilioni 116 ambazo ni sawa na mapato ya asilimia 22 ya mapato yake.

Mkurugenzi aliyesimimishwa kazi kutokea wilayani Pangani anafahamika kwa jina la Sabas Damian Chambasi.

No comments

Powered by Blogger.