DC PANGANI AWATAKA VIONGOZI KUSHIRIKIANA


Mkuu wa wilaya ya pangani bi ZAINABU ABDALLAH amewataka viongozi wa halmashauri na madiwani kushirikiana ili kutatua migogoro ya ardhi iliyopo wilayani humo.

Hayo ameyasema katika kikao cha baraza la madiwani na kusema kuwa baadhi ya mogogoro inatengenezwa na viongozi wenyewe na kuwataka kutokuweka masuala ya kisiasa  ili kupunguza idadi ya mogogoro hiyo.

‘’sasa ivi migogoro imekuwa mingi mnoo, na migogo mingine inatengenezwa na sisi wenyewe, migogoro inayoitaji ulazima mkuu wa wilaya anaenda anashiriki na anatatua migogoro, lakini mgogoro ule naumaliza nikirudi unaanzishwa tena upya, jamani tusifanye siasa kwenye mogogoro ya ardhi itatugharimu sana mimi nawaomba tushirikiane kutatua migogoro, migogoro mingine inaweza kumalizika huko huko chini waheshimiwa mpo, lakini ipo migogoro mkiiendekeza itatuharibia, pale ofisini kwangu ukilala ukiamka suala ni nini migogoro.’’

Pia Bi Zainabu amemtaka kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya pangani Bwana HAMONI NZALILA kutenga muda maalumu wa kuzungumza na wananchi ili kutatua migogoro katika maeneo yao.

‘’kaimu mkurugenzi mi naamini wewe ni afisa ardhi, mimi nataka tutenge kuanzia mwaka huu tunapoanza wiki ijayo angalau kwa wiki siku moja tutenge siku ya kusikiliza migogoro ya ardhi tuache shughuli nyingine zote tusikilize migogoro ya ardhi bila hivyo hatutawasaidia waheshimiwa madiwani watakuwa na maswali magumu ya kujibu wakati majibu tunayo sisi wataalamu, angalau kwa wiki mara moja tutenge siku kwa ajili ya kusikiliza migogoro ya ardhi na hatutakuwa tunakaa eneo moja mjini ni lazima tuzunguke, mkalamo wana migogoro, kipumbwi wana migogoro, mikinguni wana migogoro nk twendeni tukasikilize migogoro, na haya ni maagizo ya muheshimiwa waziri mkuu amesema nendeni kmasikilize migogoro.’’ 

No comments

Powered by Blogger.