OCD PANGANI ASISITIZA MALEZI MAZURI KWA WATOTO


Wazazi na walezi wilayani pangani wametakiwa kushirikiana katika malezi ya watoto wao na kuhakikisha wanawakuza katika maadili mema ili kuwaepusha na matukio ya ukatili.

Hayo yamezungumzwa na kamanda wa polisi wilayani pangani Bi Christina Musyani wakati akizungumza na Pangani Fm ofisini kwake na kusema kuwa jukumu la kuwalea watoto katika makuzi bora na salama ni la kila mwanajamii hivyo ni vyema kushirikiana ili kuangalia nyendo zao.

’Wazazi wanajukumu kubwa lakini na sisi tunahakikisha tunajukumu kubwa la kuangalia makuzi yake na nyendo zake, nia na madhumuni ni kuhakikisha kuwa wanakuwa salama, na wanakuwa katika maadili mema ambayo yanampendeza mwenyezi mungu’’.

Bi Christina amesema kuwa endapo mtoto atakutwa akizagaa mkitaani pasipo taarifa, jeshi la polisi litamchukua na mzazi/mlezi atapaswa kwenda kutoa maelezo kituoni huku akiwasihi wazazi kuwapa watoto ulinzi imara.

‘’Yeyote nitakayemuona mtoto mtaani anazagaa hana maangalizi mema na wazazi nitamchukuwa mimi, kwa hiyo tutakuja elezana vyema na wazazi, na nasema katika hilo kuna makosa katika mwenendo mzima wa makosa ya jinai kuna kutelekeza familia au kutelekeza mtoto, kuna kushindwa kumlea mtoto, sasa ukiona matoto anazagaa ujuwe umeshindwa kumle na kama umeshindwa kumlea mtoto serikali ipo na jamhuri ipo itakuelekeza namna njema ya kulea mtoto’’.

No comments

Powered by Blogger.