MAHAKAMA YA WILAYA PANGANI YAADHIMISHA SIKU YA SHERIA


Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeshauriwa kutunga sheria zenye kutoa fursa sawa na kufuta sheria kandamizi, pamoja na zile zinazochelewesha mchakato wa kupatikana kwa haki.

Hayo yamejiri katika siku ya   kilele cha Wiki ya Sheria Nchini, ambapo kwa Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga, maadhimisho hayo yamefanyika katika Viwanja vya Mahakama ya Wilaya  na kukutanisha wadau mbalimbali wa Sheria.



Katika hotuba iliyosomwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Pangani Bwana Joel Ernest Mnguto, pamoja na mambo mengine amesema kuwa Bunge linapaswa kutambua kwamba Mahakama inapaswa kutoa haki kwa mujibu wa sheria, na Bunge ndio chombo kikuu kinachotunga sheria, kwa mantiki hiyo Bunge linapaswa kusimamia Serikali ili kuhakikisha taasisi zake zinafuata utawala wa sheria.

 Bunge likumbuke kuwa Mahakama inapaswa kutoa haki kwa mujibu wa sheria na Bunge ndio chombo kikuu cha kutunga sheria, hivyo Bunge linalojukumu kubwa la kuhakikisha kuwa linatunga sheria zenye kutoa fursa sawa kwa wanaohusika kwenye mgogoro na kufuta sheria kandamizi”.

Sheria za Bunge pia zinapaswa kupunguza urasimu na mambo ya kiufundi yanayoweza kuchelewesha mchakato mzima wa utoaji haki, Bunge pia linajukumu la kusimamia serikali ili kuhakikisha taasisi zake zinafuata utawala wa sheria na haki za binaadamu” 

kuna baadhi ya sheria zimetungwa zinasababisha mlolongo fulani ambao unapelekea haki isitoke kwa wakati amesema Hakimu Mkazi Mfawidhi Pangani Bwana Joel.   



Pia amezungumzia kuhusu wadau mbalimbali wa sheria ikiwemo Jeshi la Polisi akisema wadau hao na wengine wote wanamchango muhimu katika mchakato wa kupatikana kwa haki, na kwamba katika utekelezaji wa shughuli zao wanalazimika kulinda utu wa wateja wao.

Katika hatua nyingine Bwana Joel amezungumzia changamoto mbalimbali kama Majengo, vitendea kazi na changamoto kubwa ya upungufu wa rasilimali watu ambao sio Mahakimu, kada ambazo ni muhimu pia katika kuhakikisha kazi zinafanyika kwa wakati na haki.




No comments

Powered by Blogger.