DAS PANGANI APONGEZA UFAULU WA SEKONDARI


Katibu tawala wilayani Pangani Mwalimu HASSANI NYANGE ametoa pongezi kwa waratibu elimu kata na halmashauri yote kwa matokeo mazuri ya kidato cha nne mwaka 2018 katika  shule ya sekondari Bushiri.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo Mwalimu NYANGE alisema.

‘’kwanza kabisa niwapongeze ndugu zetu wa idara ya elimu, pamoja na halmashauri kwa nafasi ambayo tumepiga naa hii inaonyesha kabisa ni kwamba japo kuwa hatukutarajia kuwa wa hamsini, lakini mipango mikakati imeshaanza, nafikiri tulikubaliana. Waheshimiwa madiwani niwaombe tutembelee shule zetu tuangalie kama waratibu kata wanafika na kama wanafanya follow up ya watoto wetu. Wao wanajukumu kubwa la kusimamia shule zetu za msingi na sekondari lakini pia wanawajibika kuwapa taarifa ya yanayoendelea kule yaani isitokee mapungufu ya walimu au changamoto za shule na wewe ukaja kuzisikia hapa wakati yeye yupo na wewe kule, kwa hiyo niwaombee muwabane na muwafuatilie’’

Aidha Mwalimu  Nyange  amewasisitizia madiwani hao kusaidia suala la chakula mashuleni kwani suala hilo linawagusa wao moja kwa moja sambamba na kutoa pongezi kwa wadau wa shule ya sekondari bushiri kwa kuanzisha bweni mapema kwa wanafunzi wao.

NYANGE amesema shule ya bushiri ni shule ya kwanza ya serikali iliyofanya vizuri na malengo ya halmashauri ni kuwa kumi bora, na kumtaka diwani wa kata ya Mwera kuupokea mpango wa kidato cha tano unaotarajiwa kuanzishwa katika kata yake.

No comments

Powered by Blogger.