TFS PANGANI YAHAMASISHA UPANDAJI MITI


Wananchi wilayani Pangani mkoani Tanga wametakiwa kujenga tabia ya upandaji wa miti katika maeneo yao ili kusaidia uhifadhi wa misitu  ya asili kwa manufaa yao na taifa.

Hayo yamezungumzwa na Meneja wa wakala wa huduma za misitu Tanzania (tfs)- Tanzania Forest Service, wilaya ya Pangani Bwana Olayce Lukumay ambapo amewataka wananchi kuanza kupanda miti kutokana na ongezeko la uvunaji wa misitu ya asili unaohatarisha kupoteza misitu hiyo.



‘’Tuwe na tabia ya kupanda miti iwe ya matunda hata ya aina gani, kwa maana kwamba mtu hatokuwa na tamaa tena ya kuingia kwenye misitu ya asili, watu wanaona kwamba miti ni mingi lakini baada ya miaka miwili au mitano shughuli ya kuirejesha itakuwa ni kubwa sana kutokana na ukataji wa sasa’’ amesema Bwana Lukumay.

Katika kufanikisha suala hilo Bwana Lukumay amesema kuwa ofisi ya wakala wa huduma za misitu wilaya ya Pangani kwa mwaka 2019/2020  wamejipanga kuzalisha miche mia mbili ya miti mbalimbali  itakayotolewa kwa wananchi wilayani humo .

‘’Tutapanda miti elfu 20 ya aina mbali mbali na miti hiyo tunatakiwa tugawe kwa wananchi wa wilaya ya Pangani kuanzia mwezi wa saba na kuendelea, itasaidia kwa kiasi kikubwa kwa maana ya kwamba tutakuwa na jamii mbali mbali ya miti na watu wenye elimu’’ amesema.

Suala la uhifadhi wa misitu katika wilayani Pangani lilikuwa na changamoto mbalimbali kutokana na wakazi wanaozunguka misitu hiyo kujihusisha na shughuli za uvunaji wa misitu kunakopelekea hatari ya kupotea kwa misitu ya asili

No comments

Powered by Blogger.