WATUMISHI PANGANI WATAKIWA KUKAZA BUTI!


Naibu waziri ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Dokta Mary Machuche Mwanjelwa amezugumzia kushuka kwa ufanisi baina ya watumishi wa umma wilayani pangani wakati wa ziara yake hivi karibuni.

Msafara wa ziara ya Naibu Waziri huyo katika ofisi ya halmashauri ya wilaya Pangani ulianzia katika ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo Bi Zainabu Abdallah Issa.

Wakati wa ziara yake Dokta Mwanjelwa amefanya kikao cha pamoja na watumishi wa umma wa ngazi mbalimbali ndani ya halmashauri hiyo akiwemo katibu tawala mkoa, Mkurugenzi wa halmashauri ya Pangani na mkuu wa wilaya ya Pangani.



Katika kikao hicho maafisa wa idara mbalimbali wamepata nafasi ya kuuliza maswali na kutoa kero na hoja mbalimbali zilizopo katika masuala ya utumishi ambapo mada mbalimbali ziliibuliwa ikiwemo utofauti wa mishahara, muundo  na uhaba wa watumishi.

‘’Najuwa hapa kuna upungufu wa watumishi, ninaelewa lakini waajiri wenu walete vibali vya kazi utumishi, sisi vibali vya maombi ya ajira vikija kwetu naomba niwaeleze kama vipo kamili kama vipo sahihi kwa wakati ndani ya miezi miwili tunakuwa tumeshatoa kibali cha ajira sisi, tunataratibu zetu, kama ni vibali vya ajira siku sitini tunakuwa tumeshatoa.’’ Amesema naibu waziri uyo

Pia Naibu Waziri Mwanjelwa alitumia nafasi hiyo kuzungumzia kushuka kwa ufanisi katika halmashauri ya wilaya Pangani.




‘’Kwenye halmashauri nyingi nikianza na halmashauri ya Pangani mambo hayakwendi, maana yake kwanza tunatakiwa tujiulize ni kwa nini mkurugenzi aliyekuwepo aliondoka nyinyi wenyewe mnaweza mkawa mnajua, sasa kwa sababu tunajua ni kwa nini mkurugenzi aliyekuwepo ameondoka, kufanya kosa sio kosa kurudia kosa ndio kosa’’ amesema Dokta Mwanjelwa.

Katika hatua nyingine Dokta Mwanjelwa ametoa maagizo kwa katibu tawala halmashauri kuunda kikosi kazi cha kufatilia mienendo ya watumishi na kuwataka watumishi wa umma kuacha kufanya kazi kimazoea

No comments

Powered by Blogger.