MAFUNZO YA UONGOZI WA MGUSO YAZIDI KUGUSA VIONGOZI


Mafunzo ya Uongozi wa Mguso yanayotolewa na shirika la UZIKWASA wilayani Pangani yametajwa kuwa ni chachu ya uongozi bora na kuleta mabadiliko chanya katika jamii na hatimaye kuifanya jamii kuwa mahala salama pa kuishi.

Akizungumza katika mafunzo saidizi yanayotolewa na shirika hilo mwenyekiti wa kijiji cha Sange Bwana Iddi Dikwanga amesema mafunzo ya mguso yamefanya uongozi wake kuwa kimbilio la jamii kwani kwa sasa anatumia nguvu shirikishi zaidi, mbinu ambayo inamfanya mwanajamii kujiona ni sehemu ya maamuzi na kuifanya jamii kuwa salama

Amesema kabla ya mafunzo hayo alikuwa anatumia ubabe, mbinu ambayo ilikuwa anajenga tabaka baina yake na wale anaowaongoza na kueleza mbinu shirikishi sio tu imeleta ukaribu baina yake na jamii bali pia imeweza kumrahishisia utendaji kazi wake.

Nae mjumbe wa kamati hiyo Ndugu Manjaa Said amesema mafunzo ya Uongozi wa Mguso yameacha alama kubwa si tu kwa jamii anayoiyongoza bali hata ndani ya familia yake na kuelezea kuwa kupitia mafunzo hayo ameweza kumshawishi kaka yake kumsomesha mtoto wake wa kike ambaye awali alikuwa hataki kumsomesha akihofia kuwa atapata ujauzito.

Aidha amesema mafunzo hayo pia yamemuwezesha kupatanisha ndugu wawili ambao walikuwa wemegombana na hawaongei kwa muda mrefu.

Hayo yamejiri katika siku moja ya mafunzo saidizi yaliofanywa na shirika la UZIKWASA katika kjiji cha Sange.

No comments

Powered by Blogger.