MADIWANI PANGANI WATAKIWA KUWA WABUNIFU

Mkuu wa Wilaya PANGANI Bi Zainab Abdalah Issa amewashauri madiwani wa kata mbalimbali za halmashauri hiyo kubuni miradi mipya ya maendeleo itakayoongeza mapato.

Hayo yamejiri katika mkutano maalum wa kujadili bajeti ya halmashauri ya wilaya ya pangani uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo.

Katika jitihada za kuongeza mapato ya halmashauri ya wilaya ya pangani mkuu wa wilaya B Zainab Abdallah issa amewashauri madiwani wa kata mbalimbali wilayani humo kubuni miradi mipya  itakayochangia kuongeza mapato ya  halmashauri.

Akizungumza katika kikao hicho kilichowakutanisha madiwani chenye lengo la kujadili na kupitisha bajeti Bi Zainab Abdalah ameshauri madiwani hao kubuni miradi mbalimbali akitolea mfano uwepo wa eneo la wazi la kuuzia vyakula na burudani mbalimbali.

‘’Lakini la pili tubuni maeneo ya vyanzo mbali mbali vya kutuingizia mapato, sisi tuna minada, lakini minada tuliyokuwa nayo ni ya kuuzia ngombe, hatuna minada hapa mjini yaani hata wiki endi huwezi kusema unakutana na nani wapi kwa ajili ya mazungumzo, hakuna sehemu ambayo unaweza kusema jamani tukutaneni hata tukachome mbuzi, kulingana na mazingira yetu inakuwa kama forodhani vile, kwa hiyo mkurugenzi mimi nikuagize hilo litatusaidia kutuingizia mapato katika halmashauri yetu’’

Pia mkuu wa wilaya alibainisha kuwa pesa za kuratibu miradi hiyo zitatoka katika ofisi ya hazina kupitia mpango serikali wa kufadhili miradi ya kimkakati katika halmashauri.

‘’Kuna miradi ya kimkakati ambayo serikali inatoa uwezeshaji bila ya malipo, yaani wanawasaidia bila ya kusema huu ni mkopo ni kama wanaandaa ufadhili serikali kuu kupitia hazina, sasa wanachokifanya wanataka miradi ambayo nyinyi halmashauri itawaingizia mapato tuu ndo kigezo chao, mtengeneze mradi muuandike mradi ambao kama milikuwa mnakusanya bilioni moja kwa hapa pangani basi mtakusanya zaidi ya hiyo, kwa hiyo sisi tunaweza tukakaa tukabuni mradi kama standi, mradi ambao utatusaidia kuingiza mapato na huyo mkishauandika uzuri tuliokuwa nao tunaweza kushawishi kule, kwa hiyo mihela iko wazi na hazina juzi wametoa zaidi ya bilioni kumi pelekeni miradi mikubwa.’’

No comments

Powered by Blogger.