MWENYEKITI WA KIJIJI APAMBANA NA MIMBA ZA UTOTONI PANGANI



Wazazi na walezi wilayani Pangani wametakiwa kuacha tamaa ya kuwaozesha watoto wao mapema kwa lengo la kujipatia fedha, badala yake wahakikishe wanawapeleka shule ili watimize ndoto zao za kielimu.

Hayo yamezungumzwa na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mivumoni Bwana Salimu MwaiPopo wakati wa mazungumzo maalumu na kituo hichi, ambapo ameongeza kuwa hivi amepata taarifa katika eneo lake kuna wanafunzi wawili ambao wanatakiwa kujiunga na kidato cha kwanza na hadi sasa hawajaripoti shuleni, wakidhaniwa kuwa wameolea.

’Hivi tamaa za kugaiwa gaiwa vitu hivi mara nyingi zinatufikisha pabaya, huwezi kujua baadae watakusaidia nini, pia tumeletewa barua kutoka kwa mkuu wa shule kuna vijana hadi sasa hawajaripoti shule wapo wawili na mmoja tunaambiwa ameondoka na baba yake wamekwenda dar es salaam wakati mtoto amefauli na hatuna taarifa zozote za kuondoka kwake’’ amesema bwana Salimu.

Aidha Bwana Mwaipopo amekemea pia tabia ya viongozi wa halmashauri ya kijiji kuvujisha taarifa za siri za serikali hali ambayo inapelekea wahalifu kutoroka.

‘’Hawa watu wana kitu kimoja wanasaidiana kwenye maovu, sasa ile inaniwia kidogo uzito kwa upande wangu, kwa sababu unaweza kuzungumza hata na mjumbe wa serikali ya kijiji kuwa kuna jambo hili, tungekuwa pamoja tumeshikana na tukasaidiana lengo lingekuwa limetimia na wahalifu wasingeweza kutoroka kwa sababu wanaovujisha siri ni wanakijiji ambao wapo katika mamlaka’’ amesema Salimu.

Inadaiwa kuwa wanafuunzi wawili wanaotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza kutoka kijiji cha Mivumoni hadi sasa hawajiropiti shuleni bila taarifa za msingi.

No comments

Powered by Blogger.