WALINZI WA (APL) PANGANI WAONJA JOTO YA JIWE


Mahakama ya mwanzo kata ya Mwera wilayani Pangani imewahukumu watu nne ambao ni walinzi wa kampuni ya Amboni Plantanion Limited (APL) tawi la Mwera kulipa faini ya shilingi laki nne kila mmoja au kifungo cha miezi sita gerezani baada ya kushindwa kuzuia kosa la wizi kutendeka.

Katika hati ya mshataka iliyowasilishwa na polisi mahakamani hapo ilidaiwa kuwa mnamo tarehe 28/01/2019 katika mashine ya mkonge yani KORONA maeneo ya Tungamaa walinzi hao walishindwa kuzuia kosa la wizi lisitendeke hivyo kupelekea kuibwa kwa brashi  yenye uzito wa kilo 158, ambapo thamani yake ni  shilingi 474,000 (LAKI NNE SABINI NA NNE ELFU) mali ya Kampuni inayojishughulisha na kilimo cha zao hilo la Mkonge ya Amboni Plantation Limited.

Mlalamikaji katika kesi hiyo Bwana Kurwa Salimu ambae ni mlinzi mkuu katika kampuni hiyo malalamiko yake ni dhidi ya Bwana Juma Adam (28), Juma Saidi (62) Joseph William (42) na Abdallah Hassan (28) ambao wote ni walinzi wa Brashi katika mashine ya mkonge huko Tungamaa na baada ya Mahakama kuwakuta na hatia wametakiwa kulipa fani hiyo ya shilingi laki nne kila mmoja pia kuilipa Kampuni hiyo fidia ya shilingi laki nne na sabini nanne elfu (474,000) kwa kuchangia wote kwa pamoja au kwenda jela miezi sita.

Kesi hiyo imesomwa chini ya Hakimu Anthony Hamza wa mahakama ya mwanzo ya kata Mwera wilayani Pangani.

No comments

Powered by Blogger.