WAVUVI PANGANI WATAKIWA KUFUATA SHERIA

Wavuvi Wilayani Pangani Mkoani Tanga wametakiwa kufuata sheria za uvuvi na endapo sheria hizo si rafiki kwao ni vyema kujenga hoja ili zifanyiwe marekebisho.

Hayo yanajiri kufuatia malalamiko ya wavuvi juu ya kile walichokiita kuwa kwa sasa wanahali ngumu ya maisha baada ya kutakiwa  kutumia nyavu za uvuvi za jicho la milimita 10 kwani hapo awali walikuwa wakitumia nyavu za jicho la milimita 8 kuvulia dagaa jambo ambalo linatajwa kuwa kinyume cha sheria.

Akizungumza katika kikao cha wavuvi kilichofanyika katika soko la samaki pangani mjini mkuu wa Wilaya ya Pangani   BI ZAINABU ABDALAH   amesema waziri hakuruhusu wavuvi kuvua na nyavu za jicho la milimita nane au sita hivyo ni vyema wavuvi wakafuata sheria wakati  viongozi wakilibeba suala hilo na kumfikishia waziri mwenye dhamana ya uvuvi.

‘’Nimesema nafunga safari naenda Dodoma, lengo yale ambayo tunaweza kumuomba waziri atumie busara katika kipindi hiki cha mpito hadi july 1 basi tumuombe na kama mengine tunaweza kuyamaliza basi tuyamalize lakini hili lazima tumshirikishe waziri mwenye  dhamana kwanza kwasababu hatuwezi kuona wananchi wetu wanateseka, biashara hazifanyiki maisha magumu tutakuja kunyoosheana vidole watu watakapo kwama kuchangia kwenye masuala ya kimaendeleo;

‘’Kwa hiyo sio kwamba haya tunayamaliza hapa hapana kuna vitu Mkuu wa Wilaya tu hawezi kuvibadili na ukilinganisha kuwa jambo lenyewe liko kisheria’’

BI ZAINABU amesema suala la faini za makosa ya uvuvi linawaumiza wananchi wa hali ya chini kwani wanachi wengi mitaji yao ni midogo hivyo ameahidi kulifikisha kwa waziri wa uvuvi.

‘’Kiuhalisia sisi kama viongozi bado wananchi wetu wanaumi na hizi faini za milioni tano kwakweli nisiwe muongo mimi mwenyewe nachangisha pesa ya matofali shilingi elfusaba miatano lakini shida ninayoipata simwambii mtu,hali ni ngumu sana kwa hiyo mimi nataka niwaahidi hili la faini tutaenda kuzungumza na waziri’’

Aidha BI Zainab   amewataka wananchi kutozichukua kero za wavuvi kama ajenda za kisiasa kwani kufanya hivyo si sahihi na  kuwataka wananchi kutofanya siasa kwenye mambo ya msingi.

BI Zainab amewataka wavuvi kusubiri majibu kutoka Wizarani ili kujua endapo wataruhusiwa kuvua na nyavu za jicho la milimita 8 au la……

No comments

Powered by Blogger.