WAKULIMA PANGANI WAHIMIZWA KUANDAA MASHAMBA


Wakulima Wilayani Pangani wametakiwa kuongeza kasi ya utayarishaji wa mashamba ili kuendana na msimu wa mvua zinazotarajiwa kunyesha hivi karibuni.

Hayo yamezungumzwa na afisa kilimo wilayani Pangani Bwana Ramadhani Zuberi wakati wa mahojiano maalumu kupitia kipindi cha Makutano kinachorushwa na  Pangani Fm na kusema kuwa kasi ya utayarishaji mashamba ni ndogo na kuwataka wakulima kujiandaa ili kuendana na msimu wa mvua.

‘’Kama wakulima wanavyojua na kwa wale wakulima wageni ni kwamba mwezi huu ni wa mwisho kwenye kutayarisha mashamba lakini nikiangalia kasi kule mashambani ni ndogo na sasa tuna wiki moja ya kufanya kazi hii ya kulima kwa sababu juzi tulikuwa kwenye kikao cha hali ya hewa na jana naona mkurugenzi katoa pia taarifa za muelekeo wa hali ya hewa ni kwamba kwa mkoa wetu wa Tanga tunatarajia kupata mvua za wastani’’amesema Afisa Kilimo

Maeongeza kuwa kuna baadhi ya mazao ambayo yanatakiwa kupandwa mwanzoni mwa msimu kabla ya mvua ili yaweze kuyalimwa mara mbili kwa mwaka na kuwataka wananchi kuhamasishana katika masuala ya kilimo.

No comments

Powered by Blogger.