ALAT MKOA WA TANGA YASISITIZA FEDHA ZA HALMASHAURI KUU KUFIKA KWA WAKATI KATIKA HALMASHAURI ZAO


Jumuiya ya serikali za mitaa  mkoani TANGA,  ALAT imefanya mkutano katika ukumbi wa halmashauri  wilayani  PANGANI mkoani humo kwa lengo la kujadili agenda mbali mbali  ikiwamo ardhi na mapato  yanayohusu halmashauri husika huku hoja kuu iliyojadiliwa na wajumbe wengi wa mkutano huo ni swala la upatikanaji wa fedha ambazo zinatoka katika halmashauri kuu kuja katika halmashauri zao kama fedha za miradi.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya HANDENI ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kikao  hicho muheshimiwa RAMADHANI DILIWA amesema kuwa fedha za miradi  ndo fedha ambazo zinaendesha halmashauri na wakati mwingine halmashauri kuu inatoa matakwa ya kuandaa bajeti ambayo inapitia sehemu mbali mbali jambo linalopelekea kutokea mabadiliko ya kufumuliwa kwa bajeti hiyo, huku akishangaa kwamba mrejesho wa mabadiliko hayo haurudi.

Ameongeza kuwa swala hilo linakwamisha shughuli za kimaendeleo ikiwemo kutokwenda kwa kasi miradi ya halmashauri hizo huku wananchi wengi wakijuwa kuwa ni uzembe wa viongozi wao na kuwataka wabunge wa wilaya zote kulibeba na kwenda kulizungumzia bungeni pamoja na kikao kikuu cha ALAT taifa ili liweze kuchukuliwa hatua.




Wajumbe kutoka Wilaya ya pangani ambao ni wenyeji wa mkutano huo walipata nafasi yakuwasilisha taarifa za miradi ya kimaendeleo zilizofuatiliwa na kamati ndogo ya wajumbe waliofanya ziara hapo jana kutoka ALAT ili kujionea hali halisi ambayo ni  mradi wa maji boza, mradi wa ujenzi wa ukingo wa mto pangani, mradi wa ujenzi wa soko, mradi wa ujenzi wa chumba cha upasuaji uliopo kijiji cha mwera ,na mradi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari funguni.

Kwa mujibu wa taarifa hizo za ukaguzi imeonekana kuwa miradi hiyo inakwenda vizuri huku changamoto kwa madarasa ya shule zikiwa ni kuta kuwa na nyufa,na komeo sio imara, na kwa upande wa mradi wa maji boza changamoto zikiwa ni kutokuwepo jenereta, na kuwataka wajumbe wa halmashauri ya pangani kuwashirikisha wananchi katika miradi yao ili kuwaongezea nguvu za uzalishaji.

Wajumbe hao wamezungumzia hali ya madeni katika kila halmashauri mkoani humo na serikali kuu ya mkoa huku wakikubaliana ifikapo desemba 31 mwaka huu kulipa madeni yote na kupeena punguzo la asilimia 50 kwa kila deni.

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya KOROGWE mkoani tanga bwana ISACK EMANUEL amezungumzia swala la wawekezaji wa makampuni ya  mkonge katika halmashauri zote ambao umeonekana kutoingizia ushuru hivyo swala hilo wameliachia wawakilishi wa mkutano mkuu kulifanyia kazi ili kupata mapato ya ndani.

Kikao hicho kimeudhuriwa na wajumbe mbali mbali wa halmashauri za mkoani tanga ikiwemo kilindi, korogwe, lushoto, tanga jiji, muheza, handeni, mkinga, korogwe vijijini, pangani ikiwa ni wenyeji wa mkutano huo huku kila halmashauri ikiwakilishwa na mwenyekiti na mkurugenzi wa halmashauri husika, na madiwani wawili.

No comments

Powered by Blogger.