WANANCHI KIJIJI CHA MWEMBENI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WAJUMBE WA KAMATI YA VMAC



Wananchi wa kijiji cha MWEMBENI wametakiwa  kushirikiana  na wajumbe  wa kamati  ya VMAC  kijijini hapo  ili kutokomeza matukio ya  ukatili   yanayowakabili  wanawake wasichana  na watoto  kijijini  hap.

Akizungumza  na Pangani Fm Mwenyekiti wa kijiji  hicho bwana MWELEKA MAHIMBURA  mbali  na  kuwataka  wananchi  kushirikiana  na  wajumbe  katika  kupunguza  matukio  hayo  amewaomba  wajumbe  wakamati kuondoa  dhana  ya   kuwa jukumu  la kutekeleza  mpango kazi  waliojiwekea ni la mtendaji na mwenyekiti  pekee.

Kwa upande wake  muwezeshaji  kutoka  shirika  la UZIKWASA   ambaye pia  ni mratibu wa masuala  ya jinsia  Bi SALVATA  KALANGA  amewataka  wajumbe hao  kufanya  juhudi za kukemea  matukio ya ukatili popote  walipo  ikiwemo kwenye nyumba za ibada ,vijiweni  na  hata  kwenye  mikutano  ya  vijiji.

Hayo  yamejiri  katika  mfululizo  wa mafunzo  ya  kupinga  ukatili  wa kijinsia  yanyoendelea  kijijini  hapo  ambapo  changamoto zilizoibuliwa  kwa siku yakwanza  zinatarajiwa  kufikishwa  kwa  wananchi kwa njia ya sanaa  za maigizo  siku  ya  mwisho ya mafunzo hayo.

No comments

Powered by Blogger.