MBUNGE WA PANGANI AWAASA WANAFUNZI WA DARASA LA SABA WANAOANZA MITIHANI YAO LEO



Mbunge wa jimbo la Pangani Mheshimiwa Jumaa Hamidu Awesso amewaasa wanafunzi wote wanaotarajia kufanya mitihani ya darasa la saba jimboni kwake kufuata sheria za mitihani hiyo ili kuhakikisha wanafanya vizuri mitihani yao.

Akizungumza na Pangani Fm Mheshimiwa Awesso amesema kuwa kufanya kwao vizuri kutawawezesha wanafunzi hao kuja kuwa wataalamu mbalimbali kama vile madaktari, waalimu na hata fani nyingine mbalimbali.

Aidha Mheshimiwa Awesso amewataka wazazi kuwatia  moyo watoto wao na pia kushirikiana vyema na waalimu ili kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakamilika  salama.

Mbunge huyo pia amesema atashirikiana na serikali ili kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu wilayani Pangani ikiwemo uhaba wa waalimu na hata miundombinu rafiki ya kufundishi.

Mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi unaanza leo kwa shule zote za msingi ambapo mitihani hii itawawezesha wanafunzi watakao chaguliwa kujiunga na shule za upili.

No comments

Powered by Blogger.