MUINGILIANO WA MAKABILA TANZANIA, FURSA NA CHANGAMOTO ZAKE




Muingiliano na mchanganyiko wa watu wa makabila tofauti imeonekana kuchangia  kupotea  kwa baadhi ya mila na tamaduni za makabila mbalimbali hususani yale yaliyohamia kutoka mkoa mmoja hadi mwingine.

Akizungumza na Pangani Fm Mzee Adam Manda ambae ni Mmakonde kutoka mkoani Mtwara, amesema kwa upande wake muda ambao amekuja mkoani Tanga ni katika kipindi ambcho alikuwa na umri wa miaka 10 kiasi cha kukosa fursa nzuri ya kujifunza juu ya mila na tamaduni za kabila lake kwa undani kutokana na kuishi na jamii nyingine.

Katika maelezo yake Mzee Adam Manda baada ya kuja mkoani Tanga na kuishi katika wilaya ya Pangani huku akifanya kazi katika shamba la mkonge, baadae aliiona kazi hiyo ni ngumu na ndipo alipoondoka na kwenda nchini Kenya ambapo huko alijishughulisha na sanaa ya vinyago ambavyo aliviuza katika hoteli za wazungu.

Wilaya ya Pangani ambayo makabila yake ya asili ni wazigua na wabondei kwa sasa ina muingiliano wa makabila mbalimbali kama vile Wabena,Waha ,Wamakonde, Wabena na makabila mengine ambapo pamoja na muingiliano huo lakini kila kabila linaheshimu kabila la mwenzake.

1 comment:

Powered by Blogger.