WANANCHI PANGANI WATAKIWA KUTII SHERIA BILA YA SHURUTI



Wananchi wilayani Pangani wametakiwa kuendelea kutii sheria bila shuruti katika sehemu zao wanazoishi   ili kuhakikisha usalama na amani unaendelea kuwepo kwa sababu suala hilo ni endelevu na halina kikomo.

Wito huo umetolea leo na Mkuu wa polisi wilaya ya Pangani Bi Christina Musyani kutokana na kuonekana baadhi matendo ya uhalifu na uvunjaji wa sheria zilizowekwa ikiwemo matukio kwa baadhi ya wanaume kuwapa mimba watoto wadogo pamoja na baadhi ya Bodaboda kutofuata kanuni za uendeshaji vyombo hivyo.

Akizungumza na Pangani fm Mkuu huyo wa Pilisi amesema kuwa vitendo vya baadhi ya wanaume kuwapa mimba wasichana wadogo, kulawiti, ubakaji na kupiga ni vitendo visivyompendeza Mungu na hata katika jami, hivyo inawapasa kujirekebisha huku akisema  jeshi la polisi linachukizwa na vitendo hivyo na litawafuatilia watu wote wanaotekelza matukio hayo ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

Pia aliwataka wanajamii kuwalinda wanafunzi wakati huu wa likizo ili kuhakikisha shule zinapofunguliwa warudi wakiwa salama na kuendelea na masomo yao.

Aidha Bi Musyani amewataka waendeshaji wa vyombo vya moto kuzingatia kanuni za usalama wa barabarani kwani waljifunza katika mafunzo yao ya udereva na kuwaonya baadhi ya waendesha pikipiki nyakati za usiku bila  kuwasha taa pamoja na kuzingatia muda wa mwisho wa kufanya kazi ya kusafirisha abiria ambao ni saa 4 usiku akionya kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka.

Kumekuwa kukitokea matokea matukio ya uvunjifu wa kanuni za usalama barabarani, ubakaji pamoja ulawiti kwa watoto katika  baadhi ya maeneo wilayani Pangani kunakotajwa kusababishwa na malezi yasiyofaa kwa baadhi ya wazazi.

No comments

Powered by Blogger.