CCM WILAYANI PANGANI WAFANYA UCHAGUZI



Jumuiya ya wazazi wilayani Pangani mkoani Tanga mwanzoni mwa wikii hii imefanya uchaguzi wa viongozi wa jumuiya hiyo ili kupata viongozi wa ngazi mbali mbali.

Akizungumza na Pangani Fm radio ofisini kwake katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilayani humo Bwana Salum Mtelela amesema mchakato wa uchaguzi huo umekwenda vizuri huku akipongeza wanachama wa chama hicho kwa kujitokeza kwa wingi katika kuwania nafasi za uongozi jambo ambalo limepelekea uchaguzi kuwa mwepesi, huru na haki katika kufanya maamuzi ya kumchagua kiongozi unayemtaka.

Kwa upande wa washindi katika uchaguzi huo ambaye ni Bi. Pili Mrefu Makwaruzo kwa nafasi ya  Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi  na Bi.  Imma Omari Kipalo kwa nafasi ya katibu elimu na malezi, wameonekana kufurahia ushindi huo huku wakiahidi kufanya kazi kwa bidii.



Wajumbe waliopata nafasi katika mkutano mkuu kitaifa ni Bi. Amina Abdallah Mwaupea, huku mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Pangani ni Bi. Mwanaidi Suleimani Mussa na Bwana Kasimu Saidi Omari kwa nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu wazazi mkoa wa tanga.

Bwana Mtelela ameendelea kutaja mjumbe wa kuwakilisha kutoka wazazi wa (UVCCM) ambaye ni Bwana. Hassani Muina Kadogo huku mjumbe mmoja kutoka wazazi kwenda UWT ni Bi. Pili Alli Msabaha.

Mwisho amemalizia kwa nafasi ya wajumbe watatu wa baraza la wazazi wilaya ya Pangani kuwa ni Sungura H. Kamaga, Mwantumu S. Makuka Na Mwanahamisi  Saidi  Rashidi.

No comments

Powered by Blogger.