WANAKIKUNDI WA KIKOBA CHA MWINDAU FOUNDATION WAHAMASIKA KUCHANGIA DAMU




Wanakikundi wa kikoba cha mwindau foundation kilichopo katika kata ya Bushiri kijiji cha msaraza Wilayani pangani hii leo wamechangia Damu salama kwa ajili ya Kuwasaidia wagonjwa wenye uhitaji wa damu kama vile mama wajawazito na watoto.
Wakizungumza mara baada ya kuchangia damu salama wamesema kuwa wamechangia kwa ajili ya kuokoa maisha ya wakina mama wajawazito,watoto na wagonjwa wengine na kuitaka jamii iwe na moyo wa kuchangia damu salama,Kwani hakuna madhara yoyote yanayoweza kuwakuta.
Kwa upande wao Kikundi cha kudhibiti ukimwi vmack msaraza kupitia mwenyekiti wake Hemedi Daudi ambao walisaidia kuwapa elimu ya uchangiaji damu kikundi cha bushiri wametanabaisha kuwa wamewahamasisha kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu salama.
Bibie Muhamedi Suleiman ni mwenyekiti wa kikundi cha mwindau foundation Ameongeza Kwa kuitaka jamii ya pangani Hususa ni wakinamama kuwa na moyo wa kuchangia damu Kwani wao ndio wenye uhitaji mkubwa wakati wa kujifungua.
Kwa kumalizia mjumbe wa kamati ya damu salama,ambaye ni msimamizi wa zoezi hilo kutoka hospital ya wilaya ya pangani Bwana peter mshabaha amesema zoezi la utoaji damu limeenda vizuri na kuwataka wananchi wawe na muamko wa kuchangia damu.
Damu salama imekuwa ni muhimu sana hususa ni kwa wakimama wajawazito hali inayopelekea,serikali kuwahamasisha wananchi kuchangia damu ili kupunguza vifo vya wakina mama.



Timu ya damu salama ikiongozwa na mratibu wa damu salama kutoka  hospitali ya wilaya ya Pangani Alhamisi  wiki hii imefanikiwa kuvuna chupa 16 za damu kwenye  zoezi la ukusanyaji wa damu  kijiji cha Meka kilichopo katika wilaya hiyo kwa lengo la kusaidia utoaji wa huduma kwa wenye mahitaji  ya damu ili kupunguza vifo vitokananvyo na upungufu wa damu.
Akizungumza baada ya kuhitimishwa kwa zoezi hilo katika kijiji cha Meka Mratibu wa damu salama wilaya ya Pangani Dokta Mfaume Salehe amewashukuru  uongozi wa kijiji hicho pamoja na wakazi wote waliojitolea damu  kwa moyo wao wa uzalendo na kusema kwamba zoezi hilo litakuwa ni endelevu  kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wenye mahitaji ya damu ikiwemo kinamama wajawazito.
Kwa upande wao wakazi waliojitokeza kuchangia damu wameelezea kufarijika kwa kuwa wamechangia damu kwa ajili ya kuwasaidia watanzania wenzao huku wakiwaomba wataalamu wa afya kutoa damu bila malipo pamoja na kendelea kuwahamasisha wanajamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu ili  kupata akiba kubwa ya damu katika hospitali hiyo.
Katika hatua nyingine Dokta Mfaume amesema ili kuongeza kiwango cha ukusanyaji damu katika wilaya ya Pangani watafanya kampeni ya kuhamasisha uchangiaji damu salama kuanzia tarehe 25 hadi 29 Mwezi huu wa tisa mwaka 2017 huku akiwaomba wananchi wahamasike katika uchangiaji wa damu.
Katika wilaya ya Pangani kumeonekana wakazi wake wameanza kuhamasika katika  kuchangia damu na kusaidia kupunguza changamoto ya wagonjwa kuhamishiwa hospitali ya Bombo kwa ajili ya kupatiwa damu .




No comments

Powered by Blogger.