ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA UBAKAJI



Jeshi la polisi wilayani PANGANI linamshikilia kijana mmoja Hermani Gwando mkulima katika mashamba ya Mkonge  mwenye umri wa miaka 32 mwenyeji wa mjini BABATI kwa kushitumiwa kumbaka mwanamke mmoja (jina limehifadhiwa ) mwenye umri wa miaka 60 mkazi wa kijiji cha MWERA wilayani humo. 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mkuu wa upelelezi wilayani Pangani SSP Eliya Matiko amesema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa tano usiku huko MWERA ambako mwanamke huyo alikuwa kwenye harusi ya ndugu yake.

Matiko ameongeza kwa kusema kuwa, baada ya kucheza  muziki kwa muda mrefu mwanamke huyo aliamua kwenda bafuni kwa ajili ya kuoga, ambapo mara baada ya kuvua nguo ndipo kijana huyo alipomvamia na kumziba mdomo na kisha kumbaka.

Tayari mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria.

No comments

Powered by Blogger.