UZIKWASA 'WAINOA' VMAC KIJIJI CHA MWEMBENI KUHUSU MALEZI NA MAKUZI YA MTOTO WA KIKE



Wajumbe wa kamati ya VMAC kijiji cha Mwembeni wamewataka wazazi na walezi wilayani PANGANI  kuachana na tabia  ya kuwatoa  wanafunzi  mimba  na badala  yake kuwasimamia katika makuzi  na malezi bora ili waweze kuwa  na ustawi mzuri wa elim.

Akizungumza  mara  baada ya mafunzo ya kuibua  changamoto za ukatili wa kijinsia  kwa wanawake, wasichana  na watoto  yanayotolewa  na shirika  la UZIKWASA mwenyekiti wa kamati hiyo Bi PILI YUSUPH ameahidi kushirikiana  na wanakamati kuwabaini wanaoshiriki katika  vitendo hivyo na kuwachukulia  hatua za kisheria na kuwataka kuaacha mara moja  kwani  inahatarisha afya za watoto.

Nae Bwana JUMAA SABURI ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo amesema kuwa vitendo hivyo ni vichafu mbele ya Mungu  na pia  wanafunzi ni lazima wawe makini  kwani jamii inawategemea katika kuwapata wataalamu wa fani mbali mbali hapa nchini .

Katika hatua nyingine  wajumbe wa  kamati hiyo wameahidi kuweka mikakati madhubuti ya kupambana na matukio yote ya ukatili  ikiwemo suala la vipigo kwa wenza ubakaji katika ndoa na utumikishwaji kwa  watototo wadog.

Hayo yote yamejiri katika mafunzo ya kupinga ukatili ambayo yanawawezesha kwa pamoja viongozi kuzama kujitafiti na kuibua matukio ya ukatili na unyanyasaji kwa wanawake  na watoto  na kuweka mpango wa pamoja  jinsi ya kumaliza matukio hayo

No comments

Powered by Blogger.