VMAC YA KIJIJI CHA MWEMBENI YAHITIMISHA MAFUNZO KWA KISHINDO




Wananchi wa kjijiji cha Mwembeni wametakiwa  kuachana na mila ambazo zinamkandamiza  na kumdhalisha  mwanamke  na mtoto  wa  kike  kijijini hapo na badala yake  kujali  utu na thamani ya mwanamke.

Akizungumza  mara  baada ya tamasha la jinsia lililofanyika kijijini hapo mjumbe  wa kamati ya VMAC  Bwana JUMAA SABURI mbali na kutaka  jamii kuachana na mila  kandamizi  ameshauri  kuendeleza mila ambazo zinazingatia  utu  na thamani ya mwanamke katika jamii. 

Akichangia  mjadala  ambao uliibuka  mara  baada  ya tamasha  hilo Bi SIKUDHANI LASMOS ambaye  ametokea katika kabila  la kimakonde  amesema kuwa  yeye  hayupo  tayari kuacha mila zake ambazo ni lazima  binti kutolewa  nje huku akiwa matiti  yako nje  na kudai kuwa utamduni huo ulikua tangu zamani  na haukuleta athari zozote kikubwa  ni mabinti kujitunza  na kuthamini utu wao.

Nae bi fatma chonya amewasihi wanajamii hiyo kuachana  na mila  kandanizi  kwaani binti kumtoa  nje  huku sehemu ya  matiti  inakuwa wazi  ni udhalilishaji wa kijinsia  na kuongeza kuwa  kitendo hiko kinaonngeza  matamanio  kwa wanaume hali ambyo inaweza  kuhgamasisha  vitendo vya ubakaji.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana MWELEKA MAHIMUBURA amewataka wanachi kushirikiana  na viongozi  katika kuondoa  matuko ya ukatili kijijini hapo.

Hayo yamejiri katika tamati  ya mafunzo ya jinsia  yanayotolewa  na shirika la uzikwasa kwa siku nne mfululizo lengo likiwa  ni kuibua  changamoto za ukatili kwa  wanawake  na watoto  na kuweka mikakati ya pamoja  kati ya viongozi  na wananchi.

No comments

Powered by Blogger.