VMAC YA MASAIKA YAIPIGA 'TAFU' KAMBI YA DARASA LA SABA KIJIJINI HAPO



Kamati ya kudhibiti ukimwi VMAC ya kijiji cha Masaika leo imeichangia kambi ya masomo ya darasa la saba ya  shule ya msingi masaika kiasi cha shilingi 29,500 kwa ajili maandilizi ya mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi kiasi hiko cha fedha,mjumbe wa kamati hiyo Bwana BAKARY MWAROGO amesema kuwa lengo la kuwasaidia ni kutaka kuwapa motisha ili wafanye vizuri katika mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi.

Naye kwa upande wake mwalimu athumani Mgeni ambaye ni mwalimu wa shule hiyo Ameongeza kuwa anaishikuru kamati hiyo kwa kusaidia fedha hizo,Hali itakayopelekea kupata aina mbali mbali ya chakula jambo ambalo litafanya wanafunzi hao kufanya vyema katika mitihani yao  ya taifa.

Shule mbali mbali wilayani pangani zimekuwa zikiwaweka kambi wanafunzi wa darasa la saba kwa ajili ya kufanya vyema katika mitihani yao ya mwisho.

No comments

Powered by Blogger.