WATOA HUDUMA ZA KIJAMII PANGANI WATAKIWA KUZINGATIA TARATIBU ZA KIAFYA ZILIZOWEKWA



Afisa wa afya wilaya Pangani Bwana JOHSEPHAT MAKOMBE amewataka watoa huduma za jamii kufuata masharti ya kisheria kama walivyoagizwa ili kuepukana na usumbufu wa kufungiwa biashara zao.

Akizungumza na Pangani Fm Bwana MAKOMBE amesema kwa sasa wapo katika zoezi la kufungia biashara ambazo hazikutimiza masharti waliotoa huku akifafanua vigezo vinavyo takiwa ili kukidhi kundesha huduma za jamii ikiwemo saluni.

Bwana MAKOMBE amesema vigezo hivyo ni chumba, ambazho kiwe na mwanga wa kutosha, kifaa cha kuzimia moto, sanduku la huduma ya kwanza, na kuwa na dawa za kusafishia vifaa hivyo.

Aidha MAKOMBE ameweka wazi suaala la kupima afya kuna fomu maalum zinazojieleza upimaji wa magonjwa, huku akisema kupima Ukimwi ni suala la maamuzi ya mhusika mwenyewe.

No comments

Powered by Blogger.