MATUKIO YA UKATILI YAPUNGUA MKWAJA, HUKU MATUMIZI YA KONDOMU KWA VIJANA YAKIIMARIKA



Wananchi wa kijiji cha MKWAJA wilayani Pangani wameeleza kupungua kwa matukio ya ubakaji na ulawiti katika kijiji chao ambayo   yaliyokuwa yakijitokeza mara kwa mara.

Wakizungumza na Pangani Fm wananchi, pamoja na mambo mengine pia wameipongeza kamati yakudhibiti ukimwi ya kijiji hicho kwa kuyashughulikia matukio ya ulawiti na ubakaji yaliyokuwa yakijitokeza hali iliyosaidia kupungua kwa vitendo hivyo viovu.

Katika hatua nyengine vijana wa kijiji hicho pia wameipongeza kamati hiyo kwa kuelimisha jamii juu ya matumizi ya kondomu huku  wakisema kwa sasa kasi ya utumiaji imeongezeka.

Vijana hao wameeleza kuwa hapo awali haikuwa rahisi kwao kukubali matumizi ya kondom lakini kutokana na juhudi za kamati hiyo kuielimisha jamii hasa vijana , mabadiliko yameanza kuonekana.

No comments

Powered by Blogger.