MAFUNZO YA UONGOZI WA MGUSO YAZAA MATUNDA KATIKA KIJIJI CHA MIKINGUNI



Mafunzo ya uwongozi wa mguso yameonekana kuwa na tija yenye kuleta maendeleo chanya katika uwongozi wa kijiji cha Mikinguni
Wakizungumza na pangani fm wajumbe wa kamati ya kudhibiti ukimwi ya Mikinguni wamesema kuwa,awali kabla hawajapatiwa mafunzo ya uwongozi wa mguso,walikosa nguvu mbadala ya kushirikiana na jamii inayowazunguka na kupelekea kuibuka kwa migogoro mbali mbali katika kijiji chao,lakini tangu wapewe elimu ya uwongozi wa mguso na shirika la Uzikwasa wameweza kutatua migogoro mbali mbali iliyopo kijijini hapo na kupelekea kujenga umoja kati ya viongozi na jamii husika.

Mbali na hayo muwakilishi kutoka katika jamii ya kifugaji ya kimasai bwana Moleli ambaye yeye pia ni mjumbe wa kamati hiyo,amesema kuwa kabla ya kupatiwa mafunzo hayo alikuwa anatumia mfumo dume katika jamii yake ya kimasai kama baba na kutumia mabavu katika maamuzi,lakina tangua ajue uwongozi wenye mguso,umemuwezesha kutoa fursa kwa wake na watoto zake kuzungumza hali inayoepusha migogoro katika familia yake

Naye kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hiko bwana salum Bungala ambaye pia mjumbe wa kamati hiyo,ametanabaisha anajiona amezaliwa upya baada ya mafunzo,na kuongeza kuwa mafunzo hayo yamemuwezesha yeye kama kiongozi kutambua uwezo na nguvu uliyondani yake jambo linalopekea kuchuku maamuzi stahaki pale kunapotokea changamoto kijiji hapo.

Mafunzo haya uwongozi wa mguso ni mafunzo yanayoendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la Uzikwasa,ni mafunzo yenye lengo la kumuwezesha kiongozi mmoja mmoja,kujitambua na kutatua changamoto zinazomzunguka kwa kutenda haki na usawa.

No comments

Powered by Blogger.