KAMATI YA VMAC KIJIJI CHA MKWAJUNI YATOA MSAADA KWA WAGONJWA WA HOSPITALI WILAYANI PANGANI



Kamati ya Kudhibiti Ukimwi Jinsia na Uongozi VMAC ya Kijiji cha Mkwajuni imefanya ziara ya kutembelea wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Pangani, kwa ajili ya kutoa msaada na kuwapa pole ikiwa ni utekelezaji wa mikakati yao kwa mwaka 2017.

Wakizungumza baada ya kukamilisha zoezi hilo Baadhi ya wawakilishi wa kamati hiyo Bi Judi Luka ambaye ni mjumbe na Bi Fatuma Mnyamisi Muhaka Afisa Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Mkwajuni, wamesema kuwa kufikia hatua hiyo ni faraja kwao kwani kwa muda mrefu walitamani kukamilisha ajenda hiyo, kama mpango uliotakiwa kukamilika ndani ya mwaka huu 2017.



‘’Nashukuru mungu kwa siku nyingi tulikuwa tunapigania kutoa msaada kwa wagonjwa wa hospitali lakini leo tumetekeleza, na tumegawa kama tulivyotarajia.’’ Mmoja wa wajumbe.

Awali wakipokea msaada huo baadhi ya wagonjwa waliopata nafasi ya kupaza sauti zao, pamoja na kuzielekeza shukrani zao kwa wanakamati hao, wahudumu wa afya na madaktari, wamesema utaratibu huo ambao jamii imejiwekea wa kuwatembelea mara kwa mara hakika inapendeza.

’Nilikuwa nasumbuliwa na tumbo lakini baada ya vipimo nimeonekana nina apendex, kwa kweli inapendeza kupata msaada huu, ninachowaombea kwa mungu awape moyo huu huu.’’ Amesema mgonjwa.



Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Mkwajuni Bi Rehema Kasimu amesema kuwa pamoja na kwamba hii ni mara yao ya kwanza, zoezi hilo litakuwa endelevu kwao huku akiwaomba wanakamati wengine kuguswa na maeneo kama magereza, hospitali na kadhalka.

’Nilipanga kuwapatia wagonjwa msaada wa sabuni na mpira kwa vijana kwa ajili ya burudani za michezo na tutawapatia leo, ninachoomba kamati nyingine kuwapatia wagonjwa msaada ili tuwape moyo, na kwa kamati yetu ya mkwajuni hii ni mara yetu ya kwanza na munmgu akipenda itakuwa ni endelevu’’ mwenyekiti wa kamati.

Naye Muhudumu wa afya katika hospitali hiyo aliyewaongoza wanakamati hao kwa kuwatembeza kila WODI Bi Mariam Ally, amesema kuwa zoezi hilo liwefunza kwa wengine kwani linaongeza upendo na faraja kwa wagonjwa.

No comments

Powered by Blogger.