WAZAZI WILAYANI PANGANI WASHAURIWA KUWEKEZA ELIMU KWA WATOTO WAO



Wazazi na walezi wilayani Pangani wameshauriwa kuwekeza kwa watoto kielimu kwa  kuwasomesha bila kuwabagua kijinsia kwa kuwa watoto wote ni sawa lakini kipaumbele kiwe kwa watoto wa kike.

 Akizungumza na wazazi waliohudhuria kwenye mahafali ya sita shule ya msingi MAKORORA wilayani humo Mhifadhi kutoka hifadhi ya Taifa SAADAN Bwana  ROMANUS MKONDA amesema elimu ndio urithi pekee kwa mtoto

‘’Somesheni watoto bila kuwabagua kama huyu ni wa kike au wa kiume lakini mimi nawashauri muwekeze zaidi kwa watoto wa kike, na sio kuwasubiri wamalize elimu yao ya msingi na kuanza kuwapeleka katika kazi za housegirl’’ amesema Mkonda.



Naye diwani wa viti maalum Mkwaja Bi HADIJA MAKATA amewataka kinamama kubadili mtazamo kutoka kwenye kununua mavazi na kuwekeza katika elimu.

‘’Kwa hiyo mama, mtoto anapomaliza shule na kufaulu vizuri kaweke rehani Madera ili mtoto aendelee na masomo kwa sababu sasa hivi elimu haichangishwi chochote ni bure kabisa, nawashauri wazazi wenzangu tufanyeni bidii katika kuwawezesha watoto kielimu na kama mtoto amefaulu hujataka kumsomesha nitahakikisha tunakwenda sambamba’’ amesema Bi Hadija.

Katika suala la mahusiano mazuri kati ya wazazi na walimu Katibu wa chama cha walimu CWT wilayani humo Mwl Ibrahim Mayunga  amewataka wazazi na walimu kuwa na ushirikiano  ilikuleta maendeleo nchini.


‘’Sasa zile zama za kale tuziache, zamani mwalimu kama mwalimu alionekana ni mgomvi na jamii na ilitokea katika baadhi ya shule sijui kata ya mkwaja, mwalimu akiwa anafundisha kuna mwingine analinda nyumba za walimu je kuna mwizi? Hizi ni zama ushirikiano kati ya walimu, wazazi na jamii kwa ujumla tushirikiane kuhakikisha mtoto anapata elimu ya uhakika’’ amesema mwalimu.

Licha ya shule yamsingi MAKORORA kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa walimu na madarasa shule HIYO imepanadai kitaaluma ambapo kwa mwaka 2016 imekuwa ya 4 kiwilaya huku mwaka 2017 ikishika nafasi ya 3 ikiwa na wanafunzi 12 waliofanya mtihani na kufanikiwa kufaulisha wanafunzi kumi watano wakike na wengine watano wakiume.

No comments

Powered by Blogger.