MSHINDI WA VMAC PANGANI KUJILIKANA KESHO



Wakazi wilayani pangani wamealikwa kufika kwa wingi katika tamasha la kupata kamati bora ya kudhibiti ukimwi jinsi na uwongozi kwa mwaka 2017 litakayofanyika  katika kijiji cha Msaraza kata ya Bushiri kesho siku ya Jumamosi ya tarehe 16/12/2017.

Akizungumza mapema hii leo na Pangani Fm Mwwezeshaji kutoka shirika la uzikwasa Bi Salvata Kalanga amesema wakazi wilayani Pangani wasisubiri kusimuliwa bali wafike kwani kujione yale yatakayojiri,huku shughuli hiyo ikitarajiwa kuanza saa tatu kamili asubuhi.

‘’Nipende katika kuwaalika watu wote ambao katika mchakato mzima wa kumtafuta mwanakamati bora wa kamati ya jinsia na uongozi , kesho ni tamati ya tamasha hili ambalo lilikuwa likisubiriwa na watu wengi  wamekuwa na kiu ya kuwa nani ataibuka kidedea na ninaomba mtu asisubiri kuambiwa na mwenzake basi asogee mwenyewe ili ajionee’’ amesema Salvata

Bi Salvata ameongeza kwa kusema maandaliza ni mazuri huku akitanabaisha kuwa  shughuli nzima itapambwa na burudani kutoka kwa wasanii wanaotaka katika maeneo mbali mbali kutoka wilaya ya Pangani
‘’Tutakuwa na burudani ambazo zinatoka ndani ya wilaya yetu, kutakuwa na muziki, ngoma za asili na mgeni rasmi tumeshampata na naamini atakuwa pamoja nasi, kwa ujumla maandalizi yako mazuri karibuni wote’’ ameongeza Salvata

Kwa upande wake Bwana Kenedy Mashema ambaye ni mwezeshaji kutoka shirika la Uzikwasa amawaalika watoto wote wiliopo katika wilayani pangani kufika katika Kijiji cha msaraza  ili waweze kuona shirika la uzikwasa linavyowapigania haki zao na huku akiongeza kuwa  kwa wale watakao shindwa kuhudhuria wategea sikio Pangani Fm radio.

‘’watoto wote kwa wilaya ya pangani mnatakiwa kuudhuria, kama hautaweza kufika katika tamasha letu basi ni vyema ukatega sikio pangani fm radio ili uweze kumsikiliza motto mwenzako ambaye ni balozi wa watoto kwa waliya ya pangani na ataelezea maswahibu yanayowakuta watoto’’ amesema Keneddy.

Shindano hilo kwa mwaka huu limebeba kauli mbiu isemayo “Lisilowezekana, Linawezekana”

No comments

Powered by Blogger.