UZIKWASA YAKUTANA NA WADAU WA ELIMU KIJIJI CHA MSARAZA WILAYANI PANGANI



Wadau wa maendeleo ya elimu na vita ya kupinga ukatili wa kijinsia waliokutana na wawezeshaji kutoka Shirika la Uzikwasa katika Kituo cha Msaraza wameonyeshwa kuwa na Imani na jitihada zinazofanywa na Shirika hilo katika kupinga masuala ya Ukatili wilayani Pangani huku wakiomba jitihada zaidi kufanyika ili kuondoa masuala ya ukatili.

Wakizungumza katika zoezi la kuwakutanisha wadau hao wamesema wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na Shirika la Uzikwasa ambapo matunda yameanza kuonekana utokana na vita dhidi ya masuala ya Ukatili huku wakishauri kuongezwe zaidi jitihada kwa kufikisha mada za ukatili kama ajenda katika mikutano ya kijiji inayofanyika kila baada ya miezi Mitatu.

‘’Suala la ukatili katika wilaya ya pangani tunatakiwa tutoe elimu ya kutosha katika kamati za vijiji ili tufikie malengo na tufikie hatua tutokomeze, elimu kubwa inatakiwa kupelekwa pia katika kamati za shule ili tupate matunda mazuri baada ya miaka miwili’’ amesema  mmoja wa wadau.



Nae Makamu Mwenyekiti wa kamati ya shule ya Msaraza Bwana IDD MAZIKA amesema kutokana na mafunzo ya Minna dada yamesaidia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha mahusiano mema kati ya wazazi, walimu na kamati pamoja na viongozi wa dini hali iliyopelekewa kufanikiwa kupunguza utoro kwa wanafunzi pamoja na kufanikiwa kutia sakafu katika baadhi ya vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Msaraza.

‘'Mimi nichukulie mafunzo ya halafu camp yameleta mabadiliko makubwa kwa vijiji vyetu mwanzo kabisa hakukuwa na cheini ya ushirikiano lakini kwa sasa cheini imekuwa nzuri kati ya wazazi, walimu na jamii na hata taasisi za lijamii, ukipata tatizo au changamoto yeyote ukiwatafuta wadau wa maendeleo yaani haichukui muda unatatuliwa changamoto yako hakika mafunzo ya alafu camp yamesaidia’’ amesema Mazika.

Katika hatua nyingine kutokana na kupata mafunzo kuhusu mfumo salama wa kuripoti matukio ya ukatili dhidi ya watoto wadau hao wameelezea yale waliofanikiwa kuyafuatilia na kuelezea mikwamo wanayokutana nayo.



‘’Kesi ilikuja kwa mwenyekiti wa kitongoji na tukamwambia hizi ni hatua za kisheria na tutafuata taratibu za kisheria kwa kuanza kumpeleka mtuhumiwa wetu polisi. Amesema Mjumbe.

Kwa upande wake mwezeshaji kutoka shirika la uzikwasa bwana Nikson Lutenda ameelezea kufarijika kwa namna wadau hao walivyoelezea maendeleo yao baada ya mafunzo kutoka shirika hilo huku akisema watafanyia kai mapendekezo walioyapata ili kutokomeza masuala ya ukatili wilayani Pangani.

‘’Kwanza katika maeneo ambayo nimevutiwa zaidi katika kijiji hichi cha msaraza ni viongozi wake wamefunguka zaidi katika kusikia uchungu, mjumbe na mwenyekiti wote wameonekana kuguswa na matatizo yanayowakabili wanafunzi, nimependa pia mahusiano yanayojengwa kati ya kamati ya shule na wazazi, kikubwa ni shirika la uzikwasa tuwe nao pamoja wadau katika kuendesha gurudumu hili la elimu’’ amesema Nickson.

Zoezi la kukutana na wadau wa maendeleo ya elimu na vita ya kupinga masuala ya ukatili wa kijinsia hufanyika kila baada ya miezi sita Kwa ajili ya kutathimini utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika la Uzikwasa kwa kushirikiana na wadau hao wa elimu.


No comments

Powered by Blogger.