"UKOSEFU WA TAARIFA SAHIHI NI HATARI WAKATI WA UJAUZITO" DOKTA MAGIRI



Ukosefu wa taarifa sahihi za mimba katika kipindi chote cha ujauzito kupitia kadi ya Clinic, kumeelezwa kusababisha hatari ikiwemo kifo kwa mama au mtoto anayetarajiwa kuzaliwa.

Hayo yamesemwa na Daktari MAGIRI EMILY kutoka kitendo cha Wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Pangani wakati akifanya mahojiani na kituo hiki, na kuongeza kuwa Jamii Wilayani humo inapaswa kufuatilia na kufahamu umuhimu wa kadi ya Clinic ya Uzazi, ili kuepuka madhara yatokanayo na uzazi.

Aidha amewashauri wazazi kujipanga katika suala la ujauzito ili kuikabili hali hiyo, hivyo ameshauri namna bora ya kuilea mimba hadi mama atakapojifungua salama.
 “Kwa jamii kikubwa kinachotakiwa kuzingatia ni kujipanga, wazazi wajipange kwenye masuala ya ujauzito, mama anapokuwa majamzito basi wazazi wote wawili wajipange kwani mimba sio ugonjwa bali ni sehemu ya maisha yetu wanadamu, kwa hiyo wajipange kikamilifu kwa namna ya kuielea hiyo mimba na namna ya jinsia mama atakavyojifungua salama” amesema Dk Magiri.

 Daktari MAGIRI amesema lengo la kutoa elimu hiyo kwa jamii ni kutokana na takwimu zao kuonyesha kiasi kikubwa cha jamii kupuuza vidokezo vilivyopo ndani ya kadi hilo kitendo kinachoweza kusababisha madhara makubwa kwa wajawazito, hivyo anatumai ya kwamba elimu hiyo itasaidia kuongeza uelewa katika jamii juu ya umuhimu wa kadi hilo.

“Tumependa kutoa hili somo kwa jamii kufahamu umuhimu wa hii kadi kwa maana ya kuzuia matatizo ya wajawazito, hii ni kutokana na takwimu zetu kwenye hospitali pamoja na vituo vyetu vinavyotoa huduma za uzazi tumeona kwamba wazazi wengi wanakuja hawajali vile vidokezo vilivyowekwa pale. Kwa hiyo lengo la sisi kama wataalam kutoa elimu hii ni kupunguza matatizo yanayojitokeza kwa wamama na watoto wanaozaliwa” amesisitiza Dk Magiri.  

Daktari huyo kutoka wodi ya wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Pangani amemalizia kwa kusema kuwa lengo lao kwa mwaka 2018, ni kuona idadi kubwa ya wanajamii wanaojua umuhimu wa kadi hilo na kulitumia ipasavyo, ili kuepuka madhara kwa mama mjamzito na mtoto anayetarajiwa kuzaliwa kwa kuhakikisha wanakuwa salama.

No comments

Powered by Blogger.