WANANCHI WILAYANI PANGANI WAMETAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA NCHI.



Wananchi wilayani Pangani wametakiwa kuzingatia sheria kwa kuzijua pamoja na kuzitii ili ziwape muelekeo wa utatuzi wa matatizo yanayowakabili.

Hayo yamezungumzwa na mwanasheria wa wilaya ya pangani bwana BARICKEL MSAKI wakati wa mazungumzo maalumu na pangani fm  na kusema kuwa iwapo mtu atazingatia sheria za nchi atakuwa na uwelewa juu ya sheria hizo na atatambua pia namna ya kuzifanyia kazi.

‘’Wito mkubwa ni kuzingatia sheria kwa sababu ukizingatia sheria utaepusha kujiingiza kwenye mikono ya sheria kwa maana kwamba sheria zinasemaje kwa kuzingatia  utiii wa sheria bila shuruti’’.amesema barickiel
Ameongeza kwa kusema kuwa pale ambapo mwananchi ametokewa na matatizo yanayoitaji masaada wa kisheria ni vyema akawatafuta wanasheria kwa wakati ili kuwasaidia kuwapa ushauri utakaowawezesha kutatua matatizo yao.

‘’Pale wanapotokewa na matatizo yanayoitaji kupata usaidizi wa kisheria kwa wakati ni vyema wakawatafuta wanasheria ili wapate usaidizi wa sheria kwa haraka’’ amesema tena msaki.

Hayo yamekuja kufuatia maadhimisho ya wiki ya msaada wa huduma za kisheria ambayo hufanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka huu kilele chake ni kesho December 8 huku yakibeba kauli mbiu isemayo ‘’umuhimu wa utoaji wa haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.

No comments

Powered by Blogger.