MVUA YASABABISHA TAMASHA LA VMAC KUTOKUFANYIKA KIJIJI CHA PANGANI MASHARIKI




Tamasha la Ukimwi, Jinsia na Uongozi lililokuwa lifanyike jana kijiji cha Pangani Mashariki katika uwanja wa Kiwanda cha Makumbi  limeshindikana kufanyika kutokana na hali ya mvua na iliyokuwa inanyesha mfululizo

Akizugumzia kuhusu hali hiyo Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana HAJI NUNDU  amesema wamelazimika kuahirisha Tamasha hilo kutokana na wakazi wa kijiji hicho kutofika katika sehemu iliyopangwa kufanyika tamasha hilo hali aliyoitaja kusababishwa na mvua.

‘’Tulipanga kufanya tamasha katika uwanja huu wa kiwanda cha makumbi lakini hali ya hewa ni ya mvua ambapo hata watu hawaja jitikeza na hata Yule tuliyempanga kwa ajili ya mziki naye anasema mziki wake ni mbovu na ndio maana tumelazimika kuhairisha mkutano huu’’ Amesema Nundu.

Aidha Bwana Haji Nundu amesema baada ya kuahirisha leo tamasha hilo wanatarajia kulifanya  siku ya Ijumaa wiki ijayo katika sehemu hiyo huku akiwataka wakazi wa kijiji hicho kuhudhuria kwa wingi siku hiyo ili kushughudia yale walioibua katika mafunzo ya Jinsia na Uongozi kijijini hapo.

‘’Sasa tujipange mungu akituwezesha siku ya ijumaa ijayo tutafanya tena tamasha hili, ninachoomba watu wajitokeze kwa wingi ili kufanikisha tamasha letu.’’ Ameongeza Nundu.

Tamasha la jinsia na uongozi  hufanyika siku nne baada ya wajumbe wa kamati ya kudhibiti ukimwi jinsia na uongozi  kupata mafunzo kwa siku tatu mfululizo ambapo wahusika katika onyesho la igizo ni wajumbe wa kamati husika iliyopatiwa mafunzo.

No comments

Powered by Blogger.