UKATILI WA KIJINSIA KUPELEKEA KASI YA MAAMBUKIZI YA VVU



Imeelezwa kuwa ukatili wa kijinsia umekuwa  kichocheo kikubwa cha ongezeko la maambukizi ya vvu katika jamii.

Hayo yamesemwa na BW NOVATUS URASA ambae ni makamu mkurugenzi wa shirika la Uzikwasa lililopo Wilayani pangani wakati dunia ikiwa katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
BW URASA amesema kuwa hapo awali shirika la uzikwasa lilikuwa likitoa elimu zaidi kwenye masuala ya ukimwi lakini kwa sasa limejikita katika kutoa elimu juu ya tabia hatarishi na matukio ya ukatili wa kijinsia yanazopelekea maambukizi ya VVU na kuwawezesha viongozi kuchukua hatua ili kupunguza kasi ya maambukizi kwani vitu hivyo vinakwenda sambamba.

“ukatili wa kijinsia kwa kiasi kikubwa sana umekuwa ukichangia maambukizi ya vvu,sisi kama shirika la uzikwasa hapo awali tulikuwa tukitoa elimu hasa katika masuala ya vvu lakini baadae tukagunduua kuwa kuielimisha jamii juu ya ukimwi bila ya kuielimisha jamii juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia ni sawa na bure kwani kwa sasa watu wanabakwa,wanalawitiwa,
 wanapigwa na kuwaathiriwa kisaikoljia hii imekuwa ikipelekea mwenza kuamua kutafuta faraja popote jambo ambalo wakati mwingine mtu huyo anaweza kuingia sehemu yoyote akiitafuta faraja bila kufikiria madhara take na kujikuta kupata maambukizi"



Adha BW URASA amewataka watanzani kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya VVU na kuacha tabia yakupuuza uwepo wa janga hilo.

“Ukimwi bado upo ,vvu bado  ipo maambukizi yako pale pale ukimwi haujasafisi ila ni kama watu wamejisahaulisha ,ujumbe tunaoutoa kupitia maadhimsho haya tunashauri tahadhari ziendee vile vile kama zilivyokuwa zikitolewa katika kipindi ambacho watu walikuwa wakiuzungumza sana na wale wanaopata maambukizi waendelee kuhudumiwa kama 
kawaida,unyayapaa usiwepo na jamii ijiepushe zaidi na ukimwi”

Tarehe mosi mwezi desember kama leo kila mwaka dunia huadhimisha siku ya ukimwi na katika Wilaya ya pangani maadhimisho hayo hanafanyika katika kijiji cha Mkaramo.

No comments

Powered by Blogger.