KIJIJI CHA PANGANI MASHARIKI CHA PIGA MARUFUKU UUZAJI WA CHAKULA ENEO LA MAGALAWANI



Serikali ya kijiji cha pangani  mashariki imepiga  marufuku  uuzwaji wa  vyakula  katika  eneo  la  magarawani   na badala yake  wafanyabiashara hao  waende katika  maeneo maalum waliopangiwa.

Akizungumza na pangani  fm kwaniaba  ya mwenyekiti wa kijiji  hicho bwana SALIMU KIRABA  ambaye  ni mwenyekiti  wa kitongoji cha funguni alisema kuwa   hali ya usafi katika eneo linalouzwa  haliridhishi  kiafya  hivyo  nivema  kutii agizo   la kuhamia  katika eneo  maalum waliotengewa.

“huu niutaratibu kwa wale  wote ambao tuliwapa  viwanja vya kufanyia biashara  hali iliyofikia  ni tete  nimefika  kwa  mama mmoja pale nikakuta amepika chakula mbele kama hatua mbili kuna jalala  hapa anapopika chakula hatua  kumi kuna choo ...na bahati nzuri  mama huyo aliwahi kupewa onyo  na maafisa wa afya kwamba asifanye biashara katika eneo hilo kwa hiyo nasema wasije kutulaumu viongozi”alisema kiraba

Aidha  bwana  KIRABA mbali  na kusisitiza  wafanyabiashara  kuhama  katika  eneo hilo  amesema kuwa  serikali  imetenga  eneo  juu kidogo na hilo (eneo la pangadeko)  kwaajili wa wanaofanya bishara kwa kuwa nisalama  kiafya  hali ambayo itaepusha   magonjwa ya mlipuko .

hili tuliliona na ndio maana  tuliwatengea  maeneo ma  kwa sababu huwezi kuuza  na chakula   wakati mwenzio anachemsha  uono ,uono una mambo mawili unatoa  maji na unamwaga  damu  hapo nzi hawawezi kukosekana  nzi atatoka hapo aende kwenye andazi la mteja  ndio mana tukasema wafanyabishara wajenge katika maeneo husika”alisema kiraba

Hayo yamejiri  baada  ya  wataalamu afya  kutembelea  eneo hilo  na kutoridhishwa  na hali ya  usafi iliyopo  na kushauri  uongozi  wa kijiji  kuwatengea  eneo  maalum wafanyabishara hao

No comments

Powered by Blogger.