HALI YA UCHUMI YATAJWA KUWA NI CHANGAMOTO KAMATI YA VMAC KIJIJI CHA MKWAJUNI WILAYANI PANGANI
Uchumi Duni kwa wajumbe wa kamati ya kudhibiti
Ukimwi Jinsia na Uongozi VMAC ya Kijiji cha Mkwajuni Wilayani Pangani,
imeelezwa kuwa ndio changamoto kubwa inayopelekea kamati hiyo kushindwa kufikia
malengo wanayojiwekea.
Akizungumza na Pangani fm Mmoja ya wajumbe wa kamati
hiyo Bwana JACOB EMMANUEL, amesema kipato duni kwenye familia nyingini za
wajumbe waliopo katika kamati yao, ni sababu inayopelekea kamati hiyo isifikie
malengo kutokana na muda mwingi wajumbe hao kuwa katika shughuli za kujiingia
kipato kwaajili ya familia.
“Kama mtu unamwambia leo twende tukafanye hivi,
lakini nyumbani kwake hakuna kitu, hawezi kwenda lazima akajitafutie rizki,
hali ya nyumbani kwake anaijua yeye. Huu ni mkwamo utamlaumu lakini sio kosa
lake, hali ya kijijini ni ngumu, uchumi wetu ni mgumu, kamati yetu inajikwamua
yenyewe, hatuna mfadhili hata mmoja” Amesema Bwana Jacob.
Aida Bwana JACOB ametaja changamoto nyingine
inayopelekea mikwamo ndani ya kamati hiyo, kuwa ni upinzani wa hali ya juu
uliopo miongoni mwa wajumbe wenyewe kiasi cha kusababisha kukosekana kwa kauli
moja katika utekelezaji wa mipango.
Hata hivyo Bwana JACOB hakusita kulimwagia sifa
shirika la UZIKWASA kutokana na juhudi zake katika kuibadilisha jamii ya
Pangani hususa“Hamuwezi nyote thelethini muende sawasawa hata kidogo, lazima na
wapinzani watakuwemo aidha kisiasa au kimaendeleo, wapo nchi nzima siwezi
kusema Mkwajuni peke yake. Baadhi ya wajumbe wanakaa kwenye vijiwe au maskani
wanazungumza mambo mabaya wakiwa pembeni, mtu anaweza akazusha jambo tu oh mimi
siji kwenye mkutano pesa zimeliwa ah! lakini mitaani unauhakika, kwahiyo
unapozungumza pembeni pale unapika sumu. Kwenye kikao na mikutano ndio kunakojenga
swali lako uliza pale pembeni haiwezekaniki” Amesisitiza Mjumbe Jacob.
ni wanawake, na kuhakikisha jamii kwa ujumla inakuwa
na uelewa wa kutosha katika dhana halisi ya UONGOZI, kujitambua, kuelewa na
kudai haki zao.
“Uzikwasa hawa watu pangani wameibadilisha, watu
wanajitambua wanaelewa maana ya uongozi kutokana na semina pamoja na mafunzo wanayotupa,
mi nasema kweli wanastahili pongezi, kwa kweli aliyebuni hili shirika sisi
hatuna cha kumlipa ila mungu hatakosa cha kumlipa. Watu hawaogopi sasa
wanafunguka wanasema, pale kwetu ilikuwa kina mama mhhh! Waoga lakini sasa
wanamihemko ya kusema hata kwenye mikutano lakini ni kwaajili ya nini semina na
mafunzo ya uzikwasa”Amesema Bwana Jacob.
Mwaka 2017, kamati za VMAC zilionekana kufanya
vizuri zaidi katika nyanja mbalimbali, ambapo pamoja na changamoto lukuki
kamati ya kijiji cha MKWAJUNI ilishika nafasi ya 3, ikiongozwa na kamati ya
MWERA iliyoshika nafasi ya 2, huku kamati Bora kwa mwaka 2017 iliyoshika nafasi
ya kwanza ni kamati ya MSARAZA.
No comments