MKANDARASI ATAKIWA KUKAMILISHA UJENZI WA JENGO LA HALMASHAURI YA PANGANI HARAKA
Mkandarasi anayeshughulikia ujenzi wa jengo jipya la
halmashauri ya wilaya ya Pangani ametakiwa kuongeza kasi ya ujenzi wa jengo
hilo ili kulikamilisha kwa wakati na
kuweza kutumika.
Maagizo hayo yametolewa leo na Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa
JOSEPHAT SINKAMBA KANDEGE wakati wa ziara yake wilayani humo, ambapo amesema ujenzi wa jengo hilo ulikuwa umesuasua kwa
muda mrefu na hivyo amemtaka mkandarasi huyo kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha
ofisi hizo.
‘’jengo
hili kama nilivyowaambia kuwa limeanza kujengwa kwa muda mrefu na taarifa
nilizokuwa nazo ni kuwa tayari halmashauri imeshapokea fedha kiasi cha shilingi
milioni mia saba lakini matumizi yake yalikuwa yanaenda kwa kusua sua sana kiasi cha mkandarasi aondoke saiti lakini leo
nimefika pale na nimemkuta, kikubwa ninachomwambia ahakikishe kuwa anafanya
haraka ili jengo la ofisi ziweze kukamilika.’’ Amesema Mh. Kandege.
Katika kuendelea na ziara hiyo mheshimiwa Naibu
Waziri JOSEPHAT KANDEGE ametembelea kituo cha Afya Kata ya Mwera ili kuona
maendeleo ya kituo hicho katika kutoa huduma ambapo mara baada ya kuona jengo
la upasuaji amesema kuwa halijajengwa kama
ilivyotakiwa na kuagiza jengo hilo likamilishwe katika kiwango kizuri.
‘’kwa
sababu jengo limeshajengwa na halikukamilika na ukitizama jengo hili limejengwa
na ramani iliyotolewa na ofisi ya Tamisemi kuna tofauti kidogo lakini tofauti
hiyo inaweza ikavumilika na kwa sababu pesa imeshatumika kiasi cha milioni ishirini na
tano (25), hatuwezi kusema pesa hii ambayo imetumika ipotee hivi hivi kwa hiyo katika hizo pesa
walizopata shilingi milioni mia nne ni pamoja na kukamilisha hiyo theater tarajiwa lakini wakamlishe kwa
kiwango kizuri’’ Amesema Mh. Kandege.
Aidha Mheshimiwa Naibu Waziri amewataka watumishi
wote wa Serilaki kupitia Halmashauri ya wilaya ya Pangani kuhakikisha
wanawajibika ipasavyo katika kuwatumikia wananchi ili kuleta maendeleo kwa
wilaya na Taifa zima kwa ujumla.
Lengo la ziara hiyo ni kukagua shughuli mbalimbali
za kimaendeleo pia na kuona namna ujenzi
wa kituo cha Afya Mwera, na kuona
maendeleo ya jengo la halmashauri ambalo ujenzi wake unaendelea.
No comments