UFAULU WA KIDATO CHA NNE PANGANI WAONGEZEKA
Siku moja baada ya Baraza la mitihani ya Taifa
Tanzania NECTA kutangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2017, imeelezwa kuwa
ufaulu kwa wanafunzi hao katika wilaya ya Pangani umeongezeka kwa asilimia
18.1 % zaidi ya mwaka 2016.
Ongezeko hilo ni kutoka asilimia 50.4 % kwa mwaka
2016 hadi kufikia asilimia 68.5% kwa mwaka 2017 ambapo wanafunzi 77
wanatarajiwa kujiunga kidato cha tano mwaka 2018 kutoka wilayani humo huku
shule za serikali zikikosa ufaulu wa daraja la kwanza.
Afisa elimu sekondari wilayani Pangani Bwana ALI
MWIN’CHAGA amezungumzia matokeo hayo
ambapo amesema pamoja na kutegemea kuwa ni ufaulu mzuri amewataka walimu
kuongeza bidii katika utoaji wa wa taalamu ili kupandisha ufaulu shule za serikal.
“Eee kwakweli walimu ndiyo wadau wakubwa haya
matokeo pamoja na kwamba tunategemea idadi hiyo kuwa ni ufaulu mzuri lakini pia
walimu waongeze bidii kwa sababu katika
shule zote saba za serikali hakuna hata shule moja yenye ufaulu wa daraja la
kwanza wanatakiwa waongeze jitihada kwakweli, ndiyo matokeo yapo juu lakini hairidhishi kwa
kiasi hicho waongeze bidii katika utoaji wa taaluma hali halisi inaonyesha.” Amesema Mwin’changa…
Aidha bwana MWIN’CHAGA amezitaja shule
tatu zilizofanya vizuri kuwa ni shule ya sekondari ALHIJIRA iliyoshika
nafasi ya kwanza, shule ya sekondari BUSHIRI nafasi ya pili, huku shule ya
sekondari FUNGUNI ikishika nafasi ya tatu, na shule ambayo imeshika nafasi ya mwisho ni sekondari ya MKWAJA huku akiitaka shule hiyo kufanya juhudi za
ziada ili kuwa na ufaulu mzuri.
“Tuna shule inayoongoza ni Alhijra na inafuata shule
ya bushiri sekondari tatu ni funguni sekondari lakini pamoja na hayo shule ya
mwisho hapo ni shule ya sekondari Mkwaja , Mkwaja haina ufaulu wa daraja la
kwanza ,wala la pili wala la tatu ina daraja la nne na daraja la sifuri kwahiyo
hawa wanahijtaji kufanya juhudi za ziada angalau wafike mbali wafike kama
wenzao, Mwaka jana angalau walitoa form five kama sikosei wawili hivi ssa mwaka
huu kwa daraja la nne wanategemea wafike kidato cha tano kweli …aah..kwahiyo
hiyo ndiyo hali halisi”. …Aliongezea
Bwana Mwin”chaga.
Kutokana na ongezeko hilo la ufaulu kwa wanafunzi
walifanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne inaonekana kwa miaka mitatu
mfululizo ufaulu katika ngazi hiyo unaendelea kupanda kila mwaka.
No comments