JESHI LA POLISI PANGANI LAKIRI KUPUNGUA MATUKIO YA UKATILI, LAKINI LASEMA KAZI BADO!
Kamanda wa
jeshi la polisi wilaya ya Pangani bi chritina musiyan hii leo ameelezea
kupungua kwa makosa ya vitendo vya ukatili yaliyo ripotiwa kutoka thalathini na
tatu kwa mwaka 2016 hadi kufikia thelathini na moja kwa mwaka 2017.
Akizungumza
na kituo hiki ofisini kwake Bi Christina amesema kuwa kwa mwaka 2017 waliweza
kupokea makosa 31 ambapo makosa nane yakiwa tayari mahakamani huku 2016 makosa
11 yalifikiswa mahakamani kati makosa 33 yaliyoripotiwa.
‘’Mwaka 2017
tuliweza kupokea taarifa za makosa haya yakiwa 31 ambapo makosa nane tayari
yalikwisha fanyiwa upelelezi na kufikishwa mahakamani, sita yanaendelea
mahakamani katika hatua tofauti na mawili tayari yalikwishafanyiwa maamuzi ya
mahakama. Na kwa mwaka 2016, tulipokea jumla ya makosa 33 ambapo makosa 11
yalifikishwa mahakamani na makosa sita yaliweza kuondolewa mahakamani, na hapa
kuna upungufu wa makosa 2 kati ya mwaka 2016 na 2017’’ Amesema OCD.
Kamanda Musyani
ameongeza kuwa hawezi kusema kuwa makosa ya ukatili Pangani yamepungua kwani
utofauti ni mdogo na pia idadi hiyo ni yale matukio yaliyoripotiwa tu kwani
bado kwenye jamii matukio yapo ila hayajafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
‘’Siwezi
kusema kwa toauti ya makosa mawili tuseme ukatili kwa Pangani haupo hapana,
hizi tunazozizungumzia ni zile kesi ambazo zimetolewa taarifa kituoni, lakini
tujuwe kwamba yapo ambayo tunayasikia kwa mbali lakini kituoni hayajafika na
pia hatuwezi kusema kuwa tumefanikiwa kwa sababu bado tatizo lipo katika kaya
zetu na katika jamii yetu ya Pangani, utofauti bado ni mdogo sana bado uwelewa
na ujasiri wa watu kuja kutoa taarifa kituoni haujafikia lengo na wengine wanakuja
kituoni kwa mihemko tu, akishakuja kutoa taarifa hajui bado kama kuna kazi au jukumu
la yeye kuja kuthibitisha.’’ Amesema Kamanda Musyani.
Aidha
kamanda Musyani amewaomba wananchi kushirikiana na jeshi la Polisi ili kila mtu
apate stahiki yake anayotakiwa kuipata kwani mtu anapopewa adhabu stahiki ni
kwa ajili ya wengine kujifunza.
‘’Tunaposema
kwamba watu washirikiane ili watu wapate adhabu ama hukumu stahiki tunamaanisha
kwanza kuifunza jamii na mtu kujifunza, watu wajue kwamba kila mtu anahitaji
kuwa huru na kila mtu ana wajibu wa kuitumia haki eneo hili la Pangani au
maeneo yoyote ili kila mtu ajifunze’’ Amesema OCD.
Licha ya
kuwepo kwa idadi ndogo ya matukio yanayo ripotiwa kituoni hapo bado baadhi ya
kesi zimeonekana kukosa ushahidi ambao utawezesha kupelekwa mahakamani jambo
ambalo linasababisha kuwepo kwa muda mrefu.
No comments