KIJIJI CHA KIGURUSIMBA WILAYANI PANGANI CHAFANYIWA MAFUNZO SAIDIZI NA SHIRIKA LA UZIKWASA
Mafunzo ya uongozi wa mguso yanayotolewa na shirika la UZIKWASA yameelezwa kuwa chachu iliyosaidia wananchi na viongozi katika kijiji cha Kigurusimba kuripoti
matukio ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia yanayojitokeza kijijini hapo.
Hayo yameelezwa
na wajumbe wa kamati ya kudhibiti ya Ukimwi Jinsia na Uongozi wakati wa mafunzo saidizi kwa kamati hiyo ambapo wajumbe hao
wamesema kuwa kwa sasa jamii ina mwamko wa kuripoti matukio hayo.
Nao baadhi ya wajumbe ya kamati hiyo wameeleza kusikitishwa na
hatua ya kuwaona wahalifu wa matukio
ya ukatili wakiwa huru mtaani badala ya
kuchukuliwa hatua za kisheria na kueleza
kuwa hali hiyo inapunguza ari na hamasa kwa wananchi
kufichua matukio hayo.
‘’Kama sisi kwetu Kigurusimba tumewekea mfano jambo
ambalo limefanyika hapa majuzi kati hatukuonyeshwa ushirikiano kwamba jambo
lile wao limewagusaje kuona kulifuatilia na kulipatia ufumbuzi hata na majibu
ya mwisho hakika na ikafanyika hatua yeyote hata sisi ambao tumepeleka taarifa
ile tukatiwa moyo kwamba jeshi la polisi linaonyesha ushirikiano na yeyote
atakayetoa taarifa. ‘’ Amesema mmoja wa
wajumbe.
Kwa upande
wake muwezeshaji kutoka shirika
la UZIKWASA Bwana FILBERT MASHINGIA amewataka wanakamati
hao kudumisha ushirikiano na
kusema kuwa ni dhahiri kuwa kamati
hiyo itafanya vizuri kwa mwaka
huu wa 2018.
‘’Ushauri wangu katika kamati ni kwamba kuendeleza
zaidi ushirikiano hata wakati tukiwa na majadiliano katika vikundi ushirikiano
ni neno mbalo limeibuka sana na wao wameweza kulithamini wakaona kwamba ni kitu
muhimu kuhusu ushirikiano kwani mpaka leo kuwepo kwa wajumbe , na baadhi ya
wenyeviti mbali mbali hata katika kipindi cha nyuma kwenye mafunzo ya uongozi
wa mguso hawakuwepo lakini leo wameweza kuwepo, imeonekana kwamba kuna umuhimu
wa wajumbe hawa kuwepo, ushauri wangu katika kamati ni kuendeleza zaidi
ushirikaino.’’ Amesema Bwana Mashingia.
Mafunzo saidizi kwa kamati za kudhibiti ukimwi VMAC hufanyika mara baada ya kamati hizo kupatiwa mafunzo ya
uongozi wa mguso.
No comments