KIPYENGA CHA UCHAGUZI KATA YA MADANGA WILAYANI PANGANI CHAPULIZWA!
Wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa Wilayani
Pangani wanaotaka kuwania kiti cha udiwani katika kata ya Madanga wametakiwa
kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea kiti hicho.
Akitoa taarifa ya kufanyika kwa uchaguzi katika kata
hiyo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bwana SABAS DAMIAN
CHAMBASI amesema kuwa zoezi la kuchukua fomu tayari limeanza tangu tarehe 14/01/2018
na linatarajiwa kukamilika tarehe 20/01/2018 mwezi huu.
‘’Ndugu wananchi tarehe ya kuchukuwa fomu ni kuanzia
tarehe 14 mpaka20, ndio itakuwa mwisho wa kuchukuwa fomu na kurejesha, lakini uchaguzi wenyewe
utafanyika tarehe 17 mwezi wa pili 2018.’’ Amesema Sabas
Pamoja na mambo mengine BW SABAS amewataka wananchi
wa kata ya Madanga waliofikia umri wa miaka 18 na wenye akili timamu kupiga
kura ya kumchagua diwani katika kata yao siku itakapo wadia.
‘’Kwa hivyo nipende kuchukuwa nafasi hii kutoa fursa
sasa kwa wananchi wote wa Pangani kwamba mnapewa fursa ya kugombea nafasi ya
uongozi kwa kata ya Madanga lakini pia ninawaomba hi wa Madanga watumie fursa
pia ya kupiga kura, wananchi waliokuwepo kata ile na walio katika orodha ya
wapiga kura wajitokeze kwa wingi kwa siku hiyo.’’ Amesema Sabas
Hatua ya kata ya Madanga kuitishwa uchaguzi inakuja
kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo SAIDI MAJIRA aliyefariki dunia
tarehe 26/11/2017
No comments