WAKULIMA PANGANI WASHAURIWA KUPANDA MAZAO YA MUDA MFUPI KIPINDI HIKI CHA MVUA
Wakulima wilayani Pangani wametakiwa kujikita zaidi
katika kilimo na kupanda mazao ya muda mfupi ili kuzitumia mvua za mwisho wa
msimu wa mwaka.
Hayo yamezungumzwa na afisa ushauri wa kilimo na
mifugo kata ya madanga Bwana RAJABU KIROKA alipokuwa akizungumza na Pangani Fm
na kusema kuwa, kuna dalili za mvua zitalazonyesha hivyo wakulima watumie fursa
hiyo kupanda mbegu za muda mfupi.
‘’Kusema kweli ni mwisho wa msimu kabisa wa mvua
lakini sasa kuna kila hali ambazo zinaonyesha kuwa kuna dalili za mvua au mvua
inanyesha na watu walishakata tamaa na mazao mengi yameathirika hususani
mahindi, kuna watu wamepanda mazao ya muda mrefu hivyo niwaambie kuwa
wachangamkie fursa ya mvua ili kupanda mazao na kupata chakula. Amesema Rajabu.
Aidha amewataka wakulima kuongeza maeneo ya kilimo
kwa kujikita zaidi katika kilimo cha Korosho ambacho kwa sasa kimekuwa na soko
ndani nan je wanchi.
‘’zao mbalo lina wika sana katika taifa letu kwa
kipindi hiki ni Korosho, hivyo shime wananchi ni kuhakikish watu wanaongeza
maeneo ya kilimo ili kuhakikisha tunatumia fursa ya zao hili lililoonekana
linafanya vizuri, tupande mikorosho kwa wingi. Ameongezea Rajabu
No comments