WALIMU WASTAAFU PANGANI WAKABIDHIWA MABATI 120 NA CWT
Walimu wastaafu wilayani Pangani wametakiwa
kufikiria ukurasa walio nao kwa kuanzisha kikundi ili kuinua na kujadili masuala
yatakayoweza kutatua changamoto za elimu wilayani humo.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa chama cha walimu
wilayani humo Mwalimu DAMIAN MACHILA wakati wa kukabidhi bati 120 kwa
wastaafu hao, ambapo mbali na hili pia amegusia suala la kutatua changamoto
iliyopo ya upungufu wa walimu Pangani.
‘’Kujitambua kwamba tupo wapi sisi kama wastaafu
kama walimu na naongea kwa niaba yenu tufikirie tunafikiria nini zaidi ya
ukurasa huu tulio nao, kwenye sikukuu ya kuagana pale nafikiri niliongelea kitu
fulani ambacho kitakuwa kama taasisi ambayo ndani yake kuna vitu tofauti
tofauti kama la kuwa na friend teachers na tuangalie tunawapata wapi, ambao
wataisaidia serikali na walimu tuliopo kazini tumezidi kupungua’’ amesema Machila.
Mwalimu MACHILA amekiri kuwamepoteza walimu wengi
wenye ubora kupitia kustaafu kwao na hivyo amewataka walimu waliobaki mashuleni
kusaidiana ili kuondokana na hali ngumu inayowakabili walimu.
‘’Hawa waliostaafu hawakustahafu kwamba hawana
akili, wamestaafu lakini bado wanauwezo wa, tumepoteza walimu wengi bora sisi tuliobaki
shuleni kwa kweli commitment ya kazi ile kubadilika kulingana na hali
inavyobadilika kuna udhaifu mkubwa sana lakini sijui tutafanyaje hali ni
ngumu’’ Amsema Machila.
Kwa upande wake Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mwalimu
Ramadhan Makunza ambaye ni Mdhiti Ubora wa elimu Pangani, licha ya kupongeza
chama cha walimu nchini pia amewapongeza wastaafu na kusema kuwa wamefanya
jambo kubwa la kuelemisha jamii.
‘’Mwalimu si kwamba ni kazi ambayo ni ya utajiri ni
kazi ya kujitolea lakini ni ya kuelimisha taifa, inawezekana kazi uliyoifanya
kwa muda wa miaka 25 hadi 30 na mmetumikia taifa kwa karibu miaka 60
ukielimisha mmoja na yule naye ataelimisha mwingine naamini umetumikia taifa na
mmefanya jambo kubwa sana katika ulimwengu huu kwa kweli tunawapongeza sana na
hata waliokuwa mawaziri mmewafundisha nyinyi’’ Amesema Makunza.
‘’Pamoja kuwa nimeshapata hela zangu nikanunua
mabati lakini bado nilikuwa na uhitaji wa haya mabati na ninachowaambia walimu
wenzangu wakiwa makazini wafanye mambo ambayo yatawasaidia walimu’’ Amesema mmoja
wa walimu hao.
Jumla ya wastaafu saba (7) wamepatiwa mabati 120 yenye
thamani ya shilingi milioni mbili laki tano na ishirini elfu ikiwa ni kwaajili
ya kuwaaga walimu hao waliostaafu kutoka kwenye shule mbalimbali wilayani
Pangani.
No comments