WADAU WA MAENDELEO PANGANI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI
Wadau wa Maendeleo katika Nyanja mbalimbali Wilayani
Pangani wameaswa kushirikiana kwa pamoja, ili kufikia adhima ya Serikali ya
Viwanda kwa kuwa na mifano halisi kiutendaji.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Pangani Bwana SABAS DAMIAN CHAMBASI kwenye Kipindi cha ASUBUHI YA LEO
kinachorushwa na kituo hiki, na kuongeza kuwa ili kuijenga Pangani ya viwanda
ni lazima wapatikane watu wenye ujuzi na maarifa katika falsafa ya viwanda.
Amesema kuwa wadau bila kubweteka, wanapaswa kuhakikisha
wanachukua hatua za makusudi kumuunga mkono Muheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli katika adhma ya serikali yake ya
kufikia uchumi wa viwanda.
‘’Tunaitaji sasa kuijenga pangani ya viwanda,
pangani ya viwanda bila kuwa na watu wenye ujuzi, bila ya kuwa na watu wenye
maarifa, na ujuzi hatuta weza, kuna kauli mbiu inayosema mkoa wetu viwanda
vyetu, sasa sisi tunasema pangani yetu viwanda vyetu, tuanze kuchukuwa hatua
kwa kumuunga mkono rais ya Tanzania ya viwanda, tusibweteke, tuhakikishe
tunathubutu kwa kuchukuwa hatua ili tufikie malengo’’ Amesema Sabas.
Bwana SABAS DAMIAN CHAMBASI ambaye ni Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Pangani, amemalizia kwa kuomba ushirikiano baina ya waheshimiwa
madiwani, watendaji wote wa halmashauri, taasisi za kiserikali na binafsi na wadau
wote wa maendeleo, kuhakikisha wanashikamana iki kuijenga pangani moja kwa
nguvu ya PAMOJA.
‘’kwanza niwatake kuwa tuungane waheshimiwa madiwani
watendaji wote wa halmashauri, pamoja na wadau wa maendeleo kama vile nmb,
uzikwasa, tanesco na taasisi mbali mbali kama bandari na tamesa ili tukakikishe
tunaijenga pangani yetu’’ amsema Sabas.
Leo kupitia
kipindi cha ASUBUHI YA LEO Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bwana
Sabas Damian Chambasi, alikuwa akitoa taarifa za utekelezaji wa mipango
mbalimbali tangu alipowasili kiutendaji katika Halmashauri hiyo mwezi wa 7
mwaka 2016 hadi Desember 31-2017, na mipango itakayotekelezwa mwaka huu mpya
2018.
No comments